Mkurugenzi wa masoko wa kampuni ya ya bia ya Serengeti Ephraim Mafuru akigonga ‘cheers’ katika uzinduzi rasmi wa msimu wa Serengeti Feista 2014. Hafla hiyo ilifanyika Serena hoteli Dar es salaam.
KAMPUNI ya bia ya Serengeti imetangaza kufungua rasmi msimu wa Serengeti Fiesta kwa mwaka huu wa 2014.
Akizungumza jijini Dare es salaam mwishoni mwa wiki katika hafla ya chakula cha jioni Mkurugenzi wa masoko wa kampuni hiyo Ephraim Mafuru alisema msimu huo wa shangwe wameutangaza rasmi baada ya kumalizika kwa mwaka uliopita wa fedha na kuanza mwingine julai mosi .
Alisema kwa mwaka huu shangwe za Serengeti Fiesta zitaanzia mkoani Mwanza na kisha kufuatiwa na mikoa mingine hapa nchini.
Aidha Mafuru alisema kuwa mbali na bia ya Serengeti ambayo ndiyo mdhamini mkuu wa Fiesta lakini pia wa watanzania wategemee kuburudika kwa bidhaa zingine mpya zinazotengenezwa na malighafi za hapa hapa nchini zitakazoingia sokoni siku chache zijazo.
No comments:
Post a Comment