RASMI wanachama wa klabu ya Simba sc wapatao 680 wamelazimika kuwafuta uanachama wanachama wenzao 72 waliokwenda mahakamani akiwemo mgombea aliyeenguliwa katika uchaguzi uliopita, ‘Kidume’ Michael Richard Wambura.
Maamuzi hayo yemefikiwa katika mkutano mkuu wa kawaida wa klabu ya Simba uliofanyika leo katika ukumbi wa Bwalo la Maofisa wa Polisi, Osterbay jijini Dar es salaam.
Mbali na wanachama kujadili masuala muhimu na kupokea taarifa mbalimbali za klabu katika mkutano huo, Agenda ya wanachama 72 waliokwenda mahakamani ndio ilibebea uzito wa juu zaidi na kila mtu alikuwa na hamu ya kutaka kujua nini hatima ya Wambura na wenzake.
Wambura aliipeleka Simba mahakamani mwaka 2010 na suala hilo lilisababisha kuenguliwa kwa jina lake katika uchaguzi mkuu wa Simba na kamati ya uchaguzi chini ya mwenyekiti wake, Wakili Dkt. Damas Daniel Ndumbaro.
Kusoma zaidi bofya www.bkmtata.blogspot.com
No comments:
Post a Comment