Thursday, February 06, 2025

WAZIRI NA NAIBU WAZIRI WA ARDHI WASHIRIKI MKUTANO WA BUNGE KWA AJILI YA KUWASILISHA TAARIFA ZA SHUGHULI ZA KAMATI

 





Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi, Mhe. Deogratius Ndejembi, pamoja na Naibu Waziri, Mhe. Geophrey Pinda, wameshiriki Mkutano wa 18 wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, ulioanza rasmi leo, Januari 28, 2025, jijini Dodoma.

Mkutano huu ni wa Kamati za Kudumu za Bunge, ambapo kila kamati inatarajiwa kuwasilisha Taarifa za mwaka za shughuli zake zilizofanyika kuanzia Januari 2024 hadi Januari 2025.

Katika kikao cha leo, Naibu Waziri Mhe. Geophrey Pinda alijibu maswali mbalimbali ya wabunge, akielezea utekelezaji wa majukumu ya wizara yake na mikakati ya kuboresha sekta ya ardhi nchini.

No comments:

WAZIRI NA NAIBU WAZIRI WA ARDHI WASHIRIKI MKUTANO WA BUNGE KWA AJILI YA KUWASILISHA TAARIFA ZA SHUGHULI ZA KAMATI

  Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi, Mhe. Deogratius Ndejembi, pamoja na Naibu Waziri, Mhe. Geophrey Pinda, wameshiriki Mkutano...