Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Philip Mpango akihutubia wakati wa ufunguzi wa Kikao Kazi cha Tano cha Serikali Mtandao kinachofanyika katika Ukumbi wa Mikutano wa Kimataifa wa Arusha (AICC). Tarehe 11 Februari 2025.
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Philip Mpango akiwa na Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora Mhe. George Simbachawene, Katibu Mkuu Ofisi ya Rais Ikulu Bw. Mululi Mahendeka, Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Serikali Mtandao (e-GA) Mhandisi Benedict Ndomba, Mkuu wa Mkoa wa Arusha Mhe. Paul Makonda katika picha ya pamoja na wajumbe wa bodi ya Mamlaka ya Serikali Mtandao (e-GA) mara baada ya ufunguzi wa Kikao Kazi cha Tano cha Serikali Mtandao kinachofanyika katika Ukumbi wa Mikutano wa Kimataifa wa Arusha (AICC) leo tarehe 11 Februari 2025.
MAKAMUwa
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Philip Mpango ametoa
rai kwa Mamlaka ya Serikali Mtandao (e-GA) kukamilisha mchakato wa
kusanifu na kujenga Mfumo Mkuu wa Ubadilishanaji Taarifa Serikalini na
kuhakikisha Taasisi zote za umma zinajumuishwa katika mfumo huo.
Makamu
wa Rais ametoa rai hiyo wakati wa Ufunguzi wa Kikao Kazi cha Tano cha
Mamlaka ya Serikali Mtandao kinachofanyika katika Ukumbi wa Mikutano wa
Kimataifa wa Arusha (AICC). Amesema Jambo hilo ni muhimu ili kurahisisha
utendaji kazi katika taasisi na kurahisisha utoaji huduma kwa wananchi
kama ilivyoelekezwa na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt.
Samia Suluhu Hassan kwa Taasisi za Umma kuhakikisha kuwa mifumo yao
inasomana na kubadilishana taarifa.
Aidha
Makamu wa Rais amesema Taasisi zote za umma zinapaswa kushirikiana na
Mamlaka ya Serikali Mtandao katika hatua zote za ujenzi au ununuzi,
usimamizi na uendeshaji wa Miradi ya TEHAMA pamoja na kuwataka
kuwaelekeza Wakuu wote wa taasisi za umma kuzingatia Sheria, Kanuni na
Miongozo inayotolewa na Mamlaka husika katika utekelezaji wa shughuli za
Serikali Mtandao.
Hali
kadhalika, Makamu wa Rais ameagiza mikoa ambayo bado haijaanza kutumia
utaratibu wa Ofisi ya Kielektroniki (e-office) kuhakikisha wanaaanza
kutumia mfumo huo ifikapo tarehe 30 mwezi juni. Aidha ameagiza kituo cha
utafiti kiweze kuimarishwa pamoja na kuongezewa eneo la ufanyaji kazi.
Makamu
wa Rais amesema Serikali itaendelea kuwekeza katika kuwajengea uwezo
wataalamu wa TEHAMA na kada nyingine, kwa kuweka mazingira wezeshi ya
ufundishaji katika Vyuo Vikuu na Taasisi za elimu ya juu ili viendelee
kuzalisha wataalam wa kutosha.
Makamu
wa Rais amewasihi washiriki wa kikao kazi hicho pamoja na Watanzania
wote kwa ujumla, ambao wana sifa za kupiga kura kushiriki katika
Uchaguzi Mkuu wa mwaka 2025 kwa kuhakikisha wanajiandikisha katika
Daftari la Kudumu la Wapiga Kura, kugombea nafasi mbalimbali za uongozi
na kushiriki kupiga kura ili kuchagua viongozi wenye sifa na uwezo
stahiki wa kusimamia na kuratibu shughuli za maendeleo katika ngazi
husika.
Kwa
upande wake Waziri Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Menejimenti ya Utumishi
wa Umma na Utawala Bora Mhe. George Simbachawene amesema lengo la kikao
hicho ni kuwakutanisha wadau mbalimbali wa serikali mtandao kutoka
katika Taasisi na Mashirika ya Umma na Sekta binafsi ili kuwapa fursa ya
kujadili hatua iliyofikiwa katika jitihada ya serikali mtandao. Amesema
kikao hicho kitaangazia mafanikio yaliyopatikana na changamoto
zinazojitokeza wakati wa utekelezaji wa jitihada hizo na namna ya
kukabiliana nazo.
Aidha
ameongeza kwamba Tanzania imepiga hatua na kupata mafanikio katika
utoaji huduma ambapo ilipata ushindi wa nafasi ya pili barani Afrika
katika Ripoti ya utafiti ya Benki ya Dunia (2022) katika nchi 198
duniani, kuhusu Ukomavu wa Matumizi ya Teknolojia Duniani katika Utoaji
wa Huduma za Serikali na Ushirikishwaji wa Wananchi (GovTech Maturity
Index).
Awali
akitoa taarifa ya kikao hicho Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Serikali
Mtandao (e-GA) Mhandisi Benedict Ndomba amesema kuanzishwa kwa mamlaka
hiyo kumeiwezesha serikali kuwa na udhibiti wa moja kwa moja wa mifumo
na miundombinu ya TEHAMA inayotumika serikalini pamoja na kulinda
usalama wa taarifa za serikali. Amesema Mamlaka ya Serikali Mtandao
hutoa msaada wa kiufundi na ushauri kuhusu usalama wa TEHAMA na
viashiria vya matishio ya kiusalama mtandaoni kwa Taasisi za Umma pamoja
na kukabiliana na mashambulio ya kimtandao pindi yanapojitokeza.
Kikao
hicho kinashirikisha zaidi ya washiriki 1300 ambapo Kauli mbiu ya kikao
kazi hicho ni “Jitihada na ubunifu wa Serikali Mtandao kwa utoaji wa
huduma za umma kwa ufanisi”.
No comments:
Post a Comment