Uongozi wa Kampuni ya uchimbaji Madini ya Shanta Mining inayomiliki mgodi wa Singida Gold Mining na New Luika umeahidi kuendelea kulipa Kodi kwa hiari na kuishukuru Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) kwa ushirikiano wanaowapa, hayo yamejili leo tarehe 05.02.2025 walipotembelewa na Kamishna Mkuu wa TRA Bw. Yusuph Juma Mwenda.
Akizungumza wakati wa ziara hiyo kwenye mgodi wa Singida Gold Mining Meneja wa Shanta Mining Company Ltd Bw. Juma Kisunda, amesema mgodini hapo wana kinu kimoja cha kuchenjua dhahabu ambacho kimekuwa na uzalishishaji wa Wakia 32,000 mpaka 36,000 kwa mwaka na kuwezesha kulipa Kodi wanayotakiwa kulipa kwa ukamilifu.
Kwa upande wake Kamishna Mkuu wa TRA Bw. Yusuph Juma Mwenda amesema lengo la kwenda mgodini hapo ni kuwashukuru Walipakodi hao na kuwataka waendelee kulipa Kodi kwa hiari huku akisikiliza changamoto zao kwa lengo la kufanya maboresho na kuweka mazingira rafiki ya ufanyaji biashara na uwekezaji.
Kamishna Mkuu Mwenda ameutaka uongozi wa Shanta Mining kuhakikisha kuwa uendeshaji wa mgodi wao unaunufaisha mkoa wa Singida kwa kupata huduma zote mkoani badala ya kuwatumia watoa huduma waliopo nje ya Singida ambao huondoka na mapato na kuwanufaisha mahala walipotoka.
No comments:
Post a Comment