Tuesday, February 11, 2025

RAIS WA ZANZIBAR AFUNGUA KITUO CHA KISASA CHA UKAGUZI NA UPASISHAJI GARI DOLE KWASILVA ZANZIBAR

Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe.Dk.Hussein Ali Mwinyi (kulia) akiondoa pazia kuweka Jiwe la Msingi la Ufunguzi wa Kituo cha Kisasa cha Ukaguzi wa Vyombo vya Moto Dole Kwasilva, Wilaya ya Magharibi “A” Unguja, ufunguzi huo uliyofanyika leo 11-2-2025.
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe.Dk.Hussein Ali Mwinyi akihutubia katika hafla ya uzinduzi wa Kituo cha Kisasa cha Ukaguzi na Upasishaji wa Gari Dole Kwasilva, uzunduzi huo uliyofanyika leo 11-2-2025 katika eneo la Dole Wilaya ya Magharibi “A” Unguja.
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe.Dk.Hussein Ali Mwinyi, akimsikiliza Mratibu wa Mradi wa Kituo cha Ukaguzi na upasishaji wa Gari Dole kwasilva Kim Lee, (kulia kwa Rais) baada ya kukifungua Kituo hicho leo 11-2-2025 kilioko katika eneo la Dole Wilaya ya Magharibi “A” Unguja na (kushoto kwa Rais) Naibu Waziri wa Ujenzi,Mawasiliano na Uchukuzi Zanzibar Mhe. Nadir Abdullatif Yussuf Al-Wardy.
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe.Dk.Hussein Ali Mwinyi, akitembelea Kituo cha Kisasa cha Ukaguzi na Upasishaji wa Gari Dole kwasilva Wilaya ya Magharibi “A” Unguja,  akimsikiliza Mratibu wa Mradi wa Kituo cha Ukaguzi na upasishaji wa Gari Dole kwasilva Kim Lee, (kushoto kwa Rais) akitowa maelezo na (kulia kwa Rais) Muwekezaji Mzalendo wa Kituo hicho cha Kisasa Mhe. Toufiq Salim Turky. baada ya kukifungua leo 11-2-2025  kilioko katika eneo la Dole Wilaya ya Magharibi “A” Unguja.

 

No comments:

RAIS WA ZANZIBAR AFUNGUA KITUO CHA KISASA CHA UKAGUZI NA UPASISHAJI GARI DOLE KWASILVA ZANZIBAR

Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe.Dk.Hussein Ali Mwinyi (kulia) akiondoa pazia kuweka Jiwe la Msingi la Ufunguzi w...