Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi, Mhe. Deogratius Ndejembi, amekutana na kufanya mazungumzo na Uongozi wa Umoja wa Wanawake Tanzania (UWT) kwa lengo la kutafuta ufumbuzi wa changamoto mbalimbali zinazokabili sekta ya ardhi nchini.
Kikao hicho kilifanyika leo, Februari 06, 2025, katika makao makuu ya Umoja wa Wanawake Tanzania (UWT) jijini Dodoma, na kuhudhuriwa na Mwenyekiti wa UWT, Mary Pius Chatanda, pamoja na Makamu Mwenyekiti wa UWT, Zainab Khamis Shomari.
Mazungumzo hayo yalijikita katika kujadili mikakati ya kuboresha ushiriki wa wanawake katika sekta ya ardhi na kuondoa vikwazo vinavyowakabili wanawake katika kumiliki na kutumia ardhi kwa ajili ya maendeleo. Mhe. Ndejembi alisisitiza umuhimu wa ushirikiano wa pande zote ili kufanikisha malengo ya kuongeza usawa na maendeleo endelevu katika sekta ya ardhi.
No comments:
Post a Comment