Sunday, February 02, 2025

WAKANDARASI WANAOJENGA BARABARA ZA TACTIC JIJINI ARUSHA KAMILISHENI UJENZI KWA WAKATI* MHANDISI MATIVILA











NAIBU Katibu Mkuu, Ofisi ya Rais Tamisemi anayeshughulikia Miundombinu Mhandisi Rogatus Mativila ameagiza wakandarasi wanaojenga barabara za Engosheraton, Olasiti na Oljoro patakapojengwa stendi mpya ya mabasi kwa Jiji la Arusha zikamilike kwa wakati.

Agizo hilo lilitolewa Jijini hapa na Mhandisi Mativila wakati alipotembelea barabara  hizo tatu zenye urefu wa kilomita 12.1 kupitia Mradi wa Kuboresha Miji  (TACTIC) uliopo chini ya TARURA.

Alisema barabara hizo tatu za Engosheraton, Olasiti na Oljoro zenye thamani ya shilingi bilioni 15.4 zinajengwa kwa kiwango cha lami lakini bado ukamilishwaji wake upo nje ya muda.

Akizungumza mara baada ya kutembelea barabara hizo Mhandisi Mativila alisema ziara hiyo ni ya kawaida katika kuangalia maendeleo ya kazi zinazofanywa katika ujenzi wa barabara hizo.

“Ujenzi wa barabara ya Oljoro bado upo nyuma kwa asilimia 35 kutokana na kubadilishwa kwa mchoro(dizaini) kutokana na kiwango chake cha usanifu na kuwa barabara ya Mkoa kutokana na ujenzi wa stendi mpya ya mabasi”.

“lakini pia barabara hii itakuwa ni kiunganishi cha barabara kuu inayoenda hadi Dodoma hapo baadaye”Aliongeza Mhandisi Mativila.

Hata hivyo alisema  tathimini ya kuongeza muda wa ujenzi wa barabara hiyo ya Oljoro imeshafanyika kwasababu mradi huo ulipaswa kukamilika mwishoni mwa mwezi huu.

"Tulipaswa kuwa asilimia 99  katika mradi huu na sasa wakandarasi wanatakiwa kukamilisha mradi huo Juni mwaka huu huku mvua zikitegemea kunyesha muda wowote hivyo lazima wakamilishe barabara hizi"

Pia alisisitiza mradi huo wa barabara hizo tatu kukamilika kwa haraka ili  Juni mwaka huu, zikabidhiwe na kusisitiza ubora ni jambo la msingi sana.

"Sijaridhika na hatua hii lakini kuna changamoto zilijitokeza hivyo wazirekebishe kwani serikali inatumia fedha nyingi katika shughuli za maendeleo hivyo lazima wasimamizi na wajenzi wa barabara hizi wakamilishe kwa wakati.

Naye, Msimamizi wa mradi huo kutoka kampuni ya ujenzi ya Mhandisi Consultant Ltd ,Mhandisi John Benedict alisema kama wahandisi wnashukuru kwa serikali kukubali changamoto hizo huku akiahidi  kwamba  mradi huo utakamilika Juni mwaka huu.

Aidha, alisema wataongeza timu ya kazi ili kupima maendeleo ya mradi anaojenga mkandarasi huyo ili kufikia malengo kwani mradi huo unatembelewa mara kwa mara huku mkandarasi analipwa kwa wakati. 

Awali Mhandisi Sofa Edward kutoka Jiji la Arusha ambao wao ndio wasimamizi wakuu aliahidi kusimamia wakandarasi hao ili wamalize kwa wakati kazi hiyo kwani wananchi wa kata hizo wanazihitaji kwaajili ya kurahisisha usafiri ikiwemo wananchi kupata maendeleo.

No comments:

WAKANDARASI WANAOJENGA BARABARA ZA TACTIC JIJINI ARUSHA KAMILISHENI UJENZI KWA WAKATI* MHANDISI MATIVILA

NAIBU Katibu Mkuu, Ofisi ya Rais Tamisemi anayeshughulikia Miundombinu Mhandisi Rogatus Mativila ameagiza wakandarasi wanaojenga barabara za...