Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Nishati na Madini, Mhandisi Paul Masanja (katikati), sambamba na Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Kimataifa la Maendeleo la Iceland (ICEIDA), Engilbert Gudmundsson, wakisaini Mkataba wa Makubaliano utakaowezesha Tanzania kunufaika na msaada wa kiasi cha Dola za Marekani 1,565,000 kwa ajili ya kupata mtaalam mwelekezi kufanya tafiti katika maeneo yenye viashiria vya Jotoardhi katika maeneo ya Luhoi na Kibiti, Mkoa wa Pwani na Kiejo/Mbaka Mkoa wa Mbeya. Wanaoshuhudia ni Meneja Mkuu wa TGDC, Mhandisi Boniface Njombe na Afisa Sheria kutoka Wizara ya Nishati na Madini Yese Malolela.
Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Kimataifa la Maendeleo la Iceland (ICEIDA), Engilbert Gudmundsson, (aliyenyoosha mkono), akieleza jambo wakati wa kikao cha kusaini wakisaini Mkataba wa Makubaliano utakaowezesha Tanzania kunufaika na msaada wa kiasi cha Dola za Marekani 1,565,000 kwa ajili ya kupata mtaalam mwelekezi kufanya tafiti katika maeneo yenye viashiria vya Jotoardhi katika maeneo ya Luhoi na Kibiti, Mkoa wa Pwani na Kiejo/Mbaka Mkoa wa Mbeya; kuwajengea uwezo wataalam wa ndani katika tasnia hiyo ikiwemo pia kuwezesha upatikanaji wa vifaa vya utafiti wa nishati hiyo. Wengine ni Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Nishati na Madini, Mhandisi Paul Masanja (katikati), wanaoshuhudia ni Meneja Mipango wa ICEIDA (kushoto), David Bjarnason, kulia ni Wataalam kutoka Wizara ya Nishati na Madini na Kampuni ya TGDC .
Mkurugenzi Mkuu wa TGDC, Mhandisi Boniface Njombe (wa kwanza kulia) akisaini Mkataba wa Makubaliano sambamba na Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Kimataifa la Maendeleo la Iceland (ICEIDA), Engilbert Gudmundsson. Mkataba huo utawezesha Tanzania kunufaika na msaada wa kiasi cha Dola za Marekani 1,565,000 kwa ajili ya kupata mtaalam mwelekezi kufanya tafiti katika maeneo yenye viashiria vya Jotoardhi katika maeneo ya Luhoi na Kibiti, Mkoa wa Pwani na Kiejo/Mbaka Mkoa wa Mbeya. Vilevile msaada huo utawezesha pia kuwajengea uwezo wataalam wa ndani katika tasnia hiyo ikiwemo na kuwezesha upatikanaji wa vifaa vya utafiti wa nishati hiyo. Wanaoshuhudia ni Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Nishati na Madini, Mhandisi Paul Masanja (katikati), Kamishna Msaidizi wa Nishati anayeshugulikia Nishati Jadidifu Edward Ishengoma (Wa kwanza kulia) na Wataalam kutoka Wizara ya Nishati na Madini na ICEIDA
Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Kimataifa la Maendeleo la Iceland (ICEIDA), Engilbert Gudmundsson (kushoto) na Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Nishati na Madini , Mhandisi Paul Masanja (kulia) wakibadilishana Mkataba wa Makubaliano utakaowezesha Tanzania kunufaika na msaada wa kiasi cha Dola za Marekani 1,565,000 kwa ajili ya kupata mtaalam mwelekezi kufanya tafiti katika maeneo yenye viashiria vya Jotoardhi katika maeneo ya Luhoi na Kibiti, Mkoa wa Pwani na Kiejo/Mbaka Mkoa wa Mbeya. Vilevile, Mkataba huo utawezesha kuwajengea uwezo wataalam wa ndani katika tasnia hiyo.
………………………………………………………………………………………………..
Na Asteria Muhozya, Dar es Salaam
Serikali kupitia Kampuni Tanzu ya Uendelezaji Jotoardhi Tanzania, (TGDC) na Shirika la Kimataifa la Maendeleo la Iceland (ICEIDA), wamesaini Mkataba wa Makubaliano utakaowezesha Tanzania kunufaika na msaada wa kiasi cha Dola za Marekani 1,565,000 kwa ajili ya kupata mtaalam mwelekezi kufanya tafiti katika maeneo yenye viashiria vya Jotoardhi; kuwajengea uwezo wataalam wa ndani katika tasnia hiyo ikiwemo pia kuwezesha upatikanaji wa vifaa vya utafiti wa nishati hiyo.
Makubaliano hayo yalifikiwa jijini Dar es Salaam, Makao Makuu ya Wizara ya Nishati na Madini, kati ya Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Nishati na Madini, Mhandisi Paul Masanja na Mkurugenzi Mkuu wa ICEIDA, Engilbert Gudmundsson, ambapo tukio hilo lilishuhudiwa na Meneja Mkuu wa TGDC, Mhandisi Boniface Njombe, Kamishna Msaidizi wa Nishati anayeshughulikia Uendelezaji wa Nishati Jadidifu, Edward Ishengoma, baadhi ya Maafisa kutoka TGDC na Wizara ya Nishati na Madini.
Akizungumza wakati wa tukio hilo, Naibu Katibu Mkuu Mhandisi Paul Masanja alisema kuwa, matarajio ya Tanzania ni kuzalisha kiasi cha megawati 200 za umeme unaotokana na nishati ya jotoardhi ifikapo mwaka 2020 ambapo taarifa za awali zinaeleza kuwa, hazina iliyopo kupitia nishati hiyo ina uwezo wa kuzalisha zaidi ya megawati elfu tano za umeme (5,000), kutokana na nishati ya jotoardhi .
Aidha, Mhandisi Masanja aliongeza kuwa, utayari na ushirikiano iliyouonesha nchi ya Iceland kupitia ICEIDA itakuwa kichocheo kikubwa kufikia malengo ya serikali ya kuwa na nishati ya kutosha ya umeme kutoka vyanzo mbalimbali.
“Tuna malengo yetu mengi kupitia nishati hii, utafiti ndio njia itakayotufanya kufikia malengo yetu hivyo, ushirikiano huu ni mwanzo mzuri kwa upande wetu. Nafahamu Iceland mlianzia katika hatua za chini kabisa lakini sasa mko mbali. Naamini uzoefu wenu utatuwezesha kuweza kufika mahali tunapotarajia,” aliongeza Mhandisi Masanja.
Aidha, Masanja aliitaka Kampuni ya TGDC, kuhakikisha inashirikiana vizuri na nchi ya Iceland ikiwemo shirika la ICEIDA kuhakikisha linafuata ushauri mzuri wa kitaalamu unaotolewa na shirika hilo ili kuweza kupata uzoefu, jambo ambalo litawezesha sekta ya jotoadhi nchini kupiga hatua na hivyo kuifanya jotoardhi kuwa chanzo kingine cha nishati ya umeme.
Kwa upande wake, Mkurugenzi Mkuu wa TGDC, Mhandisi Boniface Njombe, alishukuru utayari wa ICEIDA katika kuhakikisha kwamba Tanzania inafikia malengo yake ya kuendeleza nishati hiyo, utayari ambao utasaidia kufanyika kwa tafiti katika maeneo yenye viashiria vya jotoardhi ya Luhoi, na Kibiti, Mkoa wa Pwani.
Vilevile, Mhandisi Njombe alieleza kuwa, kutokana na utafiti utakaofanywa, utawezesha upatikanaji wa takwimu sahihi ambazo zitafungua njia ya kupata msaada zaidi kutoka katika taasisi ambazo zimejikita katika masuala ya zenye uhusiano na nishati ya jotoardhi, jambo ambalo pia litawezesha uendelezaji wa nishati hiyo nchini.
Aidha, Mhandisi Njombe alitumia fursa hiyo pia kueleza hatua mbalimbali ambazo tayari zimefanywa na kampuni hiyo katika kuhakikisha kwamba, jotoardhi inakuwa chanzo kingine cha uzalishaji umeme nchini na kuongeza kuwa, kupitia makubaliano hayo, ICEIDA itawezesha wataalam wa ndani wa TGDC kupata ujuzi na uzoefu utakaowezesha kufanyika kwa tafiti nyingine katika maeneo ya Kiejo/ Mbaka, Mkoa wa Mbeya.
Naye, Mkurugenzi wa ICEIDA, Engilbert Gudmundsson alieleza umuhimu wa nishati hiyo na unafuu wake wa gharama ikilinganishwa na nishati nyingine na kueleza kuwa, asilimia 25 ya umeme unaozalishwa nchini Iceland unatokana na nishati ya jotoardhi.
“Ilituchukua kipindi cha miaka 25 kufikia mafanikio tuliyonayo katika nishati ya jotoardhi. Kutokana na ubobezi huu ni vema kwetu kutoa uzoefu kwa TGDC kuhakikisha inafakia malengo tarajiwa na kwamba jotoardhi inakuwa chanzo kingine cha umeme kwa Tanzania ambao ni rahisi na nafuu,”aliongeza Engilbert.
Jotoardhi ni mojawapo ya chanzo cha nishati kitokanacho na mvuke unaotoka ardhini, hususan katika maeneo yaliyo katika Bonde la Ufa (Rift Valley). Nchi zilizo katika bonde la Ufa (African Rift Geothemal Facility – ARGeo) ni pamoja na Djibouti, Eritrea, Ethiopia, Kenya, Rwanda, Tanzania na Uganda.
Tayari Tanzania imefanya jitihada kadhaa za kuendeleza Jotoardhi ikiwemo uanzishwaji wa Kampuni ya TGDC, ambayo ni Kampuni Tanzu ya Shirika la Umeme nchini (TANESCO), iliyoanzishwa mwezi Juni, 2014. TGDC inatajwa kuwa kichocheo muhimu cha uendelezaji wa nishati ya jotoardhi. Aidha, mwishoni mwa mwezi Oktoba hadi mwanzoni mwa Novemba 2014, Tanzania ilikuwa Mwenyeji wa Mkutano wa Tano wa Kimataifa wa Jotoardhi uliofanyika Jijini Arusha.
Mkutano wa Jotoardhi unatajwa kuinufaisha Tanzania katika kuhamasisha matumizi ya nishati jadidifu ili kuchangia upatikanaji wa nishati hiyo nchini; kubadilishana uzoefu na uelewa na wataalamu kutoka nchi mbalimbali duniani; ikiwemo pia kuharakisha uendelezaji wa jotoardhi

No comments:
Post a Comment