Friday, December 18, 2015

WAZIRI WA NISHATI NA MADINI PROFESA SOSPETER MWIJARUBI MUHONGO ATEMBELEA KIJIJI CHA MAGOZI NA KUKAGUA VYANZO VYA MAJI MTO RUAHA

ric1
Kijiji cha Magozi chenye wakulima zaidi ya 1000 wanaolima mpunga kwa kutumia kilimo cha  umwagiliaji ambao unasababisha bwawa la mtera kukosa maji kutoka mto Ruaha kwa sababu za kilimo cha umwagiliaji. Pamoja na wakulima Hawa pia wapo wakulima  wa Mbalali mkoa wa Mbeya ambao wote kutokana na shughuli hizo za kilimo husababisha ufuaji umeme kukwama katika bwawa la  Mtera na Kidatu  mkoani Morogoro.
Waziri wa Nishati na Madini Profesa Sospeter Mwijarubi Muhongo kushoto anayezungumza na Richard Kasesela Mkuu wa wilaya ya Iringa  alitembelea  bonde hilo na kukagua shughuli za kilimo zinazoendelea katika bonde hilo na kusababisha upotevu wa maji katika mto Ruaha ambao unapeleka maji katika mabwawa ya kufua umeme Mtera, Mkuu wa wilaya ya Iringa ameitisha mkutano wa wadau wote  siku ya jumatatu tarehe  21 mwezi huu . ili kufanya majadiliano na kupanga mkakati wa Kuokoa bwawa la Mtera.
ric2
Waziri wa Nishati na Madini Profesa Sospeter Mwijarubi Muhongo akikagua eneo hilo na Mkuu wa Wilaya ya Iringa Mh. Richard Kasesela leo.
ric3
Waziri wa Nishati na Madini Profesa Sospeter Mwijarubi Muhongo akizungumza na baadhi ya wakulima hao wakati alipokagua bonde hilo kulia anayemsikiliza ni Mkuu wa wilaya ya Iringa Mh. Richard Kasesela.
ric4
Waziri wa Nishati na Madini Profesa Sospeter Mwijarubi Muhongo akizungumza na mkuu wa wilaya ya Iringa Mh. Richard Kasesela wakati alipotembelea bonde la Usangu lenye shughuli za kilimo cha Umwagiliaji.
ric5
Mkuu wa wilaya ya Iringa Mh. Richard Kasesela akimwelezea jambo waziri wa Nishati na Madini wakati alipokagua bonde la Usangu katika kijiji cha Magozi chenye wakulima wa mpunga zaidi ya 1000.

No comments:

WIZARA YA ARDHI YAPONGEZWA KUTENGA FEDHA KUKAMILISHA MRADI WA MAKTABA

Kamati ya Bunge ya Ardhi, Maliasili na Utalii imeipongeza Wizara ya Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi kwa kutenga fedha kiasi cha Shiling...