Katibu Mkuu Wizara ya Fedha na Mipango Dkt. Servacius Likwelile (wa kwanza kushoto) akitoa ufafanuzi kwa Waziri wa Fedha na Mipango Mhe. Dkt Philip Mpango (wa pili kulia) mara baada ya kuwasili Wizarani hapo jana jijini Dar es salaam. Wa kwanza kulia ni Naibu Waziri wa Fedha na Mipango Mhe. Dkt. Ashatu Kijaji.
Naibu Katibu Mkuu anayeshughulikia Sera Prof. Adolph Mkenda akifafanua jambo ofisini kwa Waziri wa Fedha na Mipango Mhe. Dkt. Philip Mpango mara baada ya kuwasili Wizarani hapo jana jijini Dar es salaam.
Naibu Waziri wa Fedha na Mipango Mhe. Dkt. Ashatu Kijaji akitoa taarifa fupi kwa Waziri wa Fedha na Mipango Mhe.Dkt. Philip Mpango (wa kwanza kulia) ikiwa ni sehemu ya ukaribisho kwa Waziri huyo Wizarani hapo.
Watendaji wa Wizara ya Fedha na Mipango wakielezea majukumu ya Idara na Vitengo katika mkutano na Waziri wa Fedha na Mipango Mhe.Dkt. Philip mara baada ya kuwasili Wizarani hapo jana jijini Dar es salaam.
Waziri wa Fedha na Mipango Mhe. Dkt. Philip Mpango akionesha kadi aliyoipokea kutoka kwa viongozi kwaniaba ya watumishi wa Wizara hiyo yenye lengo la kumpongeza kwa kuteuliwa kushika wadhifa huo. Wa kwanza kulia ni Kaibu Mkuu Wizara ya Fedha na Mipango Dkt. Servacius Likwelile na Mkurugenzi Idara ya Utawala na Rasilimaliwatu Bi. Deodatha Makani (katikati).
(Picha na Kitengo cha Mawasiliano Wizara ya Fedha na Mipango)
(Picha na Kitengo cha Mawasiliano Wizara ya Fedha na Mipango)
,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,
Watumishi Wizara ya Fedha na Mipango wameaswa kufanya kazi kwa weledi na kuwekeza nguvu zaidi katika ukusanyaji mapato ili kukuza uchumi wa nchi na kuifanya nchi iwe kitovu cha uchumi Barani Afrika.
Hayo yamesemwa na Waziri wa Fedha na Mipango Mhe. Dkt. Philip Mpango alipokuwa akiongea na watendaji wa Wizara hiyo alipowasili Wizarani hapo mara baada ya kuapishwa jana Ikulu jijini Dar es salaam.
Katika mazungumzo yake na watendaji hao, Mhe. Dkt. Mpango, aliuagiza uongozi wa Wizara yake kuunda na kisimamia sera za mfumo wa ukusanyaji kodi ambao utabaki kuwa rafiki kwa wafanyabiashara ili kukuza biashara na uwekezaji nchini.
“Ili kutekeleza kutekeleza ukusanyaji wa kodi kwa kutumia mfumo rafiki kwa wafanyabiashara na Serikali, Wizara inawajibu wa kusimamia na kukuza uchumi ambao utawanufaisha wananchi walio wengi, kwa kuhakikisha kodi zote ndogondogo ambazo ziko chini na nje ya Wizara, ambazo ni kero kwa wanachi wa hali ya chini zinapatiwa ufumbuzi kwani wananchi hao nao wanastahili maisha mazuri” Alisema Mhe. Dkt. Mpango.
Waziri Dkt. Mpango aliwasisitiza watendaji kufanya kazi kwa bidii, maarifa na weledi ili nchi iweze kupiga hatua kwa kuzingatia nidhamu katika kufanya kazi ambayo ni dhamana walizokabidhiwa.
Naye Naibu Waziri Wizara ya Fedha na Mipango Mhe. Dkt. Ashatu Kijaji aliwahimiza watendaji wa wizara hiyo kufanyakazi kwa umoja na mshikamano waliokuwa nao katika utendaji kazi ili kuleta maendeleo yenye tija huku akisisitiza kuwa wizara hiyo ndiyo msingi katika kukuza uchumi wa nchi.
Kwa upande wake Katibu Mkuu Wizara ya Fedha na Mipango na Mlipaji Mkuu wa Serikali, Dkt. Servacius Likwelile aliwapongeza Viongozi hao wapya wa Wizara kwa kuteuliwa kwao kuiongoza Wizara ambayo ndiyo muhimili wa Serikali.
Aidha, Dkt. Likwelile alitoa wito kwa watendaji wa wizara hiyo kuzingatia maagizo ya Mhe. Waziri kwa maendeleo ya nchi ili kulinda hadhi na heshima ya wizara.
Imetolewa na Kitengo cha Mawasiliano
Wizara ya Fedha na Mipango
28 Desemba, 2015
No comments:
Post a Comment