Kampuni
ya Tigo Tanzania hivi karibunii metangaza kufikisha wafuasi milioni moja katika
mtandao wao wa Facebook. Katika ukarasa wake wa facebook, www.facebook.com/TigoTanzania kampunii lifikisha mfuasi wa milioni moja Jumapili Desemba
27 mwaka huu hapa Tanzania.
Kutokana
na ongezeko la matumizi ya mtandao wa kijamii wa Facebook hapa nchini, Facebook
imekuwa mstari wa mbele katika matumizi kutokana uzinduzi wa Facebook katika lugha
ya Kiswahili uliofanyika mwaka wa 2014 kwa ushirikiano wa Tigo Tanzania na
Facebook, ambapo wateja wanaweza kutumia Facebook kwa lugha ya Kiswahili na Kiingereza
kupitia simu zao za mkononi bila malipo yoyote ya ziada.
Ukurasa
wa Facebook wa Tigo uliundwa Juni 2011 na umekuwa jukwaa madhubuti wa kurambaza
na wateja wake wapendwa ambapo wanajifunza kuhusu huduma na bidhaa mpya za kampuni.
Hivi
karibuni, Tigo Tanzania imejishindia tuzo
mbili katika Tuzo za Uongozi Bora (Tanzania Leadership Awards) ambayo inatambua
mashirikana watu binafsi katika uongozi.
Tuzo hizo ni ya Ubora wa bidhaa (The Hall of Fame in Brand Excellence),
na Matumizi Bora yaMitandao ya Kijamii KatikaMauzo ( Best use of Social Media in Marketing).
Tigo
Tanzania inaongoza katika soko la mawasiliano na imekuwa mstari wa mbele katika
mitandao ya kijamii ambapo wateja wamekuwa wakiuliza maswali na kujibiwa haraka.
Hii
imeufanya mtandao kuaminika sana na wateja na kutumika kama mwendelezo wa huduma
kwa wateja.
Kuhusu
Facebook Mkurugenzi wa Tigo Bwana Diego Gutierrez anasema. “Jukwaaletula Facebook
na Twitter (Tigo TZ) limekuwa kitendea kazi muhimu ambacho kinatumika kujifunza
kutoka kwa wateja wetu na jamii kwa jumla ambao wanakitumia.
Tunajivunia kwakuweza
kuyafikia mafanikio haya, na tunawashukuru wateja wetu kwa kuwa na imani nasi.
Tigo imedhamiria kubadilisha mtindo wa maisha wa kidijitali
kwa kuwaletea wateja wetu ubunifu wa teknolojia maridhawa. Hivikaribuni,
tumezindua teknolojia ya 4G LTE hapa Tanzania ambayo ni intaneti iliyo na kasi kuliko
zote pamoja na ofa ya aina ya simu yaTechno Y3 Smartphone inayotumia lugha ya Kiswahili.
No comments:
Post a Comment