Sunday, December 20, 2015

NAPE AWAAMBIA WANA MASASI KUICHAGUA CCM LEO KWANI NDIO CHAMA AMBACHO ILANI YAKE INATEKELEZWA

 Katibu wa NEC Itikadi na Uenezi ambaye pia ni Mbunge wa Jimbo la Mtama(CCM) na Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Mhe. Nape Moses Nnauye akihutubia wakazi wa Masasi kwenye mkutano wa kufunga kampeni uliofanyika Mkomaindo kata ya Mkomaindo ambapo aliwaambia wakazi wa Masasi watambue kuwa ilani inayotekelezwa ni Ilani ya CCM hivyo kuwapa jimbo wapinzani ni sawa na kuliweka rehani kwani hakuna sera ya mpinzani itakayotekelezwa kwa kipindi cha miaka 5, aliwataka wananchi hao kutofanya makosa na kuhakikisha wanamchagua mgombea wa CCM ili aendane sawa na kasi ya Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dk. John Pombe Magufuli.
 Katibu wa NEC Itikadi na Uenezi ambaye pia ni Mbunge wa Jimbo la
Mtama(CCM) na Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Mhe. Nape
Moses Nnauye akisisitiza wananchama wa CCM hasa wakina Mama kujitokeza kwa wingi kwenda kupiga kura na kuwahakikishia usalama utakuwa wakutosha.
Katibu wa NEC Itikadi na Uenezi ambaye pia ni Mbunge wa Jimbo la
Mtama(CCM) na Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Mhe. Nape
Moses Nnauye akimnadi mgombea ubunge wa CCM jimbo la Masasi Ndugu Rashid Chuachua  katika viwanja vya Maendeleo, Mkomaindo, Masasi.
 Mgombea Ubunge wa Jimbo la Masasi kwa tiketi ya CCM Bw. Rashid Chuachua akihutubia wakazi wa Masasi waliojitokeza kwa wingi kwenye mkutano wa kufunga kampeni za ubunge jimboni hapo.
 Mbunge wa Jimbo la Mtwara Vijijini (CCM) Mhe. Hawa Ghasia akihutubia wakazi wa Masasi kwenye mkutano wa kufunga kampeni za ubunge ambapo aliwaambia wakazi hao kumpa kura za kutosha Bw. Rashid Chuachua.
 Mbunge wa Jimbo la Newala mjini (CCM) Mhe. George Mkuchika akihutubia wakazi wa Masasi kwenye kilele cha kufunga kampeni za ubunge jimbo hilo zilizofanyika Mkomaindo
 Wakazi wa Masasi wakishangilia sera za CCM kwenye mkutano wa kufunga kampeni.
Wasanii maarufu wa muziki wa kizazi kipya Mabaga Fresh wakitumbuiza kabla ya kuanza kwa mkutano wa mwisho wa kampeni za CCM ambapo nao walisisitiza kwa wananchi kumpigia kura mgombea ubunge kupitia CCM Bw. Rashid Chuachua.

No comments:

WIZARA YA ARDHI YAPONGEZWA KUTENGA FEDHA KUKAMILISHA MRADI WA MAKTABA

Kamati ya Bunge ya Ardhi, Maliasili na Utalii imeipongeza Wizara ya Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi kwa kutenga fedha kiasi cha Shiling...