Thursday, December 17, 2015

WAZIRI WA AFYA, MAENDELEO YA JAMII, JINSIA WAZEE NA WATOTO, MHE. UMMY MWALIMU AZINDUA BODI MPYA YA TAASISI YA SARATANI YA OCEAN ROAD.


Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Mhe. Ummy Mwalimu (katikati) akipokelewa na Kaimu Mkurugenzi wa Hospitali ya Saratani ya Ocean Road, Bwana Diwan Msemo (kushoto) mara alipowasili katika Hospitali ya Saratani ya Ocean Road ya Jijini Dar es Salaam kwenye Uzinduzi wa Bodi ya Taasisi ya Saratani ya Ocean Road uliofanyika leo 17 Desemba, 2015.
Kaimu Mkurugenzi wa Hospitali ya Saratani ya Ocean Road, Bwana Diwan Msemo (aliyevaa suti) akimpeleka Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Mhe. Ummy Mwalimu (kulia) katika chumba ambacho ukarabati wa mashine za matibabu zilizopata hitilafu ukiendelea katika Hospitali hiyo mara alipowasili hospitalini hapo mapema 17 Desemba, 2015.
Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Mhe. Ummy Mwalimu (wa pili kulia) akipatiwa maelezo toka kwa Mganga wa Hospitali ya Saratani ya Ocean Road juu ya matatizo ya kiufundi ilizozikumba mashine za matibabu hospitalini hapo wakati wa ziara yake 
ya Uzinduzi wa Bodi ya Taasisi ya Saratani ya ya hospitalini hapo uliofanyika leo 17 Desemba, 2015. Kulia ni Kaimu Mkurugenzi wa Hospitali ya Saratani ya Ocean Road, Bwana Diwan Msemo
Baadhi ya Mafundi wakionekana kutengeneza mashine iliyopata matatizo wakati wa ziara ya Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Mhe. Ummy Mwalimu hospitalini hapo iliyolenga kufanya Uzinduzi ikiwemo kuangalia vitendea kazi na kero wazipatazo wagonjwa wenye matatizo ya saratani katika Hospitali ya Saratani ya Ocean Road.
Kaimu Mkurugenzi wa Hospitali ya Saratani ya Ocean Road, Bwana Diwan Msemo (kulia) akimpeleka Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Mhe. Ummy Mwalimu (katikati) kuangalia jengo ambalo litatumika kwa ajili ya mashine maalum za kufanyia huduma za mionzi kwa wagonjwa wa saratani katika Hospitali hiyo.

No comments:

WIZARA YA ARDHI YAPONGEZWA KUTENGA FEDHA KUKAMILISHA MRADI WA MAKTABA

Kamati ya Bunge ya Ardhi, Maliasili na Utalii imeipongeza Wizara ya Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi kwa kutenga fedha kiasi cha Shiling...