Sunday, December 20, 2015

UMMY AWATAKA HALMASHAURI KUDHIBITI UPOTEAJI WA DAWA

x9
Waziri wa Afya,Maendeleo ya Jamii,Jinsia,Wazee na Watoto,Ummy Mwalimu akiongea na Uongozi wa Mkoa wa Tanga,Waziri Ummy yupo mkoani Hapa kwenye ziara ya kikazi sehemu ya afya na wazee.
x8
Naibu Waziri, Ofisi ya Rais (Tamisemi, Utumishi na Utawala Bora),Seleman Jaffo (Kulia) na Katibu Tawala wa Mkoa wa Tanga, Salum Chime kwenye  ukumbi wa Mkuu wa Mkoa,
x10
Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii,Jinsia,Wazee na Watoto akisaini kitabu cha wageni kwenye Ukumbi wa Mkuu wa mkoa.
x11
Waziri Ummy Mwalimu akiwa na Mkuu wa Wilaya ya Tanga Abdullah Lutari (wa pili Kulia) na afisa toka wizara ya afya Dkt. Ibrahim Maduhu.
………………………………………………………..
Na. Catherine Sungura,WAMJW-Tanga
Halmashauri zote nchi zimetakiwa kujitahidi kudhibiti upoteaji wa dawa na vifaa tiba kwenye vituo vya afya ili wananchi waweze kupata tiba sahii na inayostahili
Hayo yamesema leo na Waziri wa Afya,Maendeleo ya Jamii,Jinsia,Wazee na Watoto Ummy Mwalimu wakati alipokutana na Uongozi wa Mkoani hapa.
Ummy alisema kumekuwa na upoteaji dawa na vifaa tiba mara vifikapo kwenye vituo vya afya kwa kuzunguka na kupelekwa kuuzwa kwenye maduka ya dawa na hospitali binafsi
Alimtaka Mganga mkuu wa mkoa kudhibiti upoteaji wa dawa kwa kutoa elimu kwa kamati ya afya juu ya majukumu yao ili dawa zote zinazowafikia zisipotee mikononi mwa watu wachache.
“Nimejifunza kuwa dawa zinapopokelewa kwenye vituo zinazunguka tena na kwenda kwa wauzaji binafsi hivyo hakuna udhibiti wa uingiaji na utokaji wa dawa na hivyo kufanya dawa nyingi kupotea kwenye maduka ya dawa binafsi
Aidha alisema ataongea na Bohari ya dawa (MSD) ili kuanzisha utaratibu wa kila dawa zinazopelekwa kwenye kituo ziwe zinabandikwa kwenye ubao wa matangazo wa vituo vyote nchini ili wananchi wajue dawa zilizopo kwenye kituo chake nia aina gani.
Hata hivyo amemuomba Naibu Waziri, Ofisi ya Rais(Tamisemi,Utumishi na Utawala Bora),Seleman Seleman Jaffo kuwachukulia hatua pamoja na kusisitiza suala la nidhamu,uwajibikaji na uadilifu kwa watendaji hususan kwenye sekta ya afya, kwakuwa yeye hana dhamana ya kuwasimamisha kazi moja kwa mojaWaganga wakuu wa mikoa na Wilaya kwakuwa yeye anasimamia sera na miongozo ya sekta ya afya.

No comments:

WIZARA YA ARDHI YAPONGEZWA KUTENGA FEDHA KUKAMILISHA MRADI WA MAKTABA

Kamati ya Bunge ya Ardhi, Maliasili na Utalii imeipongeza Wizara ya Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi kwa kutenga fedha kiasi cha Shiling...