Tuesday, December 29, 2015

NAIBU WAZIRI MASAUNI APOKELEWA NA WATUMISHI WA WIZARA YA MAMBO YA NDANI YA NCHI

mas1
Naibu waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi Mh. Hamad Masauni wa pili kushoto akipokelewa na Katibu Mkuu wa  wizara hiyo Mbarak Abdulwakil wa watatu kulia mara baada ya Naibu waziri huyo kupokea Ua alilokabidhiwa na watumishi wa wizara hiyo ikiwa ni ishara ya kukaribishwa wizarani hapo  baada ya Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dk. John Magufuli kumuapisha kushika wadhifa huo Ikulu jana jijini Dar es Salaam.
mas2
Naibu waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi Mh. Hamad Masauni wa kwanza kushoto akisalimiana na Kamisha wa Operesheni na Mafunzo wa Jeshi la Polisi Paul Chagonja wa pili kulia muda mfupi baada ya Naibu waziri huyo kukaribishwa wizarani hapo baada ya Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dk. John Magufuli kumuapisha kushika wadhifa huo Ikulu jana jijini Dar es Salaam wa kwanza kulia ni Mkurugenzi Mtendaji wa Mamlaka ya Vitambulisho vya Taifa (NIDA).
mas3
Naibu waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi Mh. Hamad Masauni wa pili kushoto akisalimiana na Kamisha wa Utawala na Fedha wa Jeshi la Magereza Gaston Sanga wa pili kulia muda mfupi baada ya Naibu waziri huyo kukaribishwa wizarani hapo mara tu baada ya kuapishwa Ikulu jana jijini Dar es Salaam.
mas4
Mkurugenzi wa Utawala na Usimamizi wa Rasilimali Watu Lilian Mapfa watatu kulia  akimkaribisha Naibu waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi Mh. Hamad Masauni wa pili kushoto muda mfupi baada ya Naibu waziri huyo kukaribishwa wizarani hapo mara tu baada ya kuapishwa Ikulu jana  jijini Dar es Salaam wa pili kulia ni Mkurugenzi Msaidizi wa Idara ya Huduma kwa Jamii.
mas5
Sehemu ya watumishi wa wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi kushoto wakimpokea Naibu waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi Mh. Hamad Masauni wa tatu kulia muda mfupi baada ya Naibu waziri huyo kukaribishwa wizarani hapo mara tu baada ya kuapishwa Ikulu jana jijini Dar es Salaam.
mas6
Naibu waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi Mh. Hamad Masauni akisaini kitabu baada ya kupokelewa katika wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi muda mfupi baada ya kuapishwa na Rais wa Jamhuri ya muungano wa Tanzania Mh. John Magufuli Ikulu jana  jijini Dar es Salaam.
mas7
Katibu Mkuu wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi hiyo Mbarak Abdulwakil  wa kwanza kulia akimfafanulia jambo  Naibu waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi Mh. Hamad Masauni  baada ya Naibu waziri huyo kupokelewa  na watumishi wa wizara hiyo mara tu baada ya kuapishwa Ikulu jana jijini Dar es Salaam.
mas8
Naibu waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi Mh. Hamad Masauni akisalimiana na baadhi ya Wakurugenzi na Wakurugenzi Wasaidizi wa wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi mara baada ya Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kumuapishwa jana kushika nafasi hiyo katika hafla iliyofanyika Ikulu jana jijini Dar es Salaam.

No comments:

WIZARA YA ARDHI YAPONGEZWA KUTENGA FEDHA KUKAMILISHA MRADI WA MAKTABA

Kamati ya Bunge ya Ardhi, Maliasili na Utalii imeipongeza Wizara ya Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi kwa kutenga fedha kiasi cha Shiling...