Saturday, May 09, 2015

TANZANIA KUTIBU MARADHI YA MOYO BILA KUFANYA UPASUAJI

Baadhi ya Waandishi wa habari wakifanya kazi yao na kuelekezwa namna (Cath Lab) mtambo wa kufanya uchunguzi na kuzibua mishipa ya damu inayopeleka damu kwenye moyo na pia kuziba matundu ndani ya moyo bila kufungua kifua.
Katikati ni Kaimu Mkurugenzi Mtendaji wa Hospitali ya Taifa Muhimbili Dkt. Hussein Kidanto akizungumza na waandishi wa habari. Kushoto ni Prof. Jameel Alata ambaye ni Daktari Mwelekezi wa Magonjwa ya Watoto ambaye ameongoza timu ya madaktari bingwa kutoka Hospitali ya Prince Sultan Cardiac Centre iliyoko Riyadhi nchini Saudi…
Baadhi ya Waandishi wa habari wakifanya kazi yao na kuelekezwa namna (Cath Lab) mtambo wa kufanya uchunguzi na kuzibua mishipa ya damu inayopeleka damu kwenye moyo na pia kuziba matundu ndani ya moyo bila kufungua kifua.
Katikati ni Kaimu Mkurugenzi Mtendaji wa Hospitali ya Taifa Muhimbili Dkt. Hussein Kidanto akizungumza na waandishi wa habari. Kushoto ni Prof. Jameel Alata ambaye ni Daktari Mwelekezi wa Magonjwa ya Watoto ambaye ameongoza timu ya madaktari bingwa kutoka Hospitali ya Prince Sultan Cardiac Centre iliyoko Riyadhi nchini Saudi Arabia ambao watakuwepo Muhimbili kwa siku tisa kuanzia tarehe 8 hadi 16 Mei, mwaka huu. Kulia ni Sheikh Said Ahmed Abri ambaye ni Mwenyekiti Mtendaji wa Shirika lisilo la Kiserikali la Kiislam la hapa nchini liitwayo Dhi Nureyn Islamic Foundation na shirika hili ndilo lililoratibu timu hii ya madaktari kuja kutoa huduma.

Baadhi ya madaktari bingwa kutoka Hospitali ya Prince Sultan Cardiac Centre iliyoko Riyadhi nchini Saudi Arabia wakimsikiliza Kaimu Mkurugenzi Mtendaji wa Hospitali ya Taifa Muhimbili wakati akiwakaribisha na kuzungumza na vyombo vya habari, leo Jijini Dar Es Salaam.
Mwezi Mei tarehe 9, mwaka 2015, Tanzania imeandika historia nyingine baada ya kufanya Tiba ya moyo bila ya kufanya upasuaji kwa kuziba matundu yaliyoko kwenye moyo kwa kutumia “kifaa maalum” bila kufungua kifua kama ilivyozoeleka.
Tiba hii inafanyika kwa mara ya kwanza nchini kupitia Idara ya Tiba na Upasuaji Moyo ya Hospitali ya Taifa Muhimbili ikishirikiana na madaktari bingwa kutoka Hospitali ya Prince Sultan Cardiac Centre iliyoko Riyadhi nchini Saudi Arabia ambao watakuwepo Muhimbili kwa siku tisa kuanzia tarehe 9 hadi 16 Mei, mwaka huu.
Madaktari hawa wamekuja kupitia taasisi ya Al Mutanda Islami Trust ya Uingereza. Akizungumza na wanahabari, Kaimu Mkurugenzi Mtendaji wa Hospitali ya Taifa Muhimbili Dkt. Hussein Kidanto amesema jumla ya wagonjwa zaidi ya 20 wanatarajiwa kupatiwa tiba hii.
CHANZO: MICHUZI

No comments:

RAIS SAMIA AONGOZA KIKAO CHA BARAZA LA MAWAZIRI DODOMA

  Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan akiongoza Kikao cha Baraza la Mawaziri kilichofanyika Ikulu Chamwin...