Mkuu wa Mkoa wa Pwani Injinia Evarist Ndikilo akimpokea Mke wa Rais na Mwenyekiti wa Taasisi ya Wanawake na Maendeleo, WAMA, Mama Salma Kikwete wakati alipowasili kwenye uwanja wa mpira wa Shule ya Sekondari Nyamisati iliyoko wilayani Rufiji kwa helicopter tarehe 2.5.2015. Mama Salma alikwenda Rufiji kwenye tamasha la Elimu ya Afya ya Uzazi kwa vijana katika Shule ya Sekondari ya WAMA-Nakayama ambayo inamilikiwa na Taasisi ya WAMA ambapo Mkuu wa Mkoa wa Pwani alikuwa Mgeni Rasmi.
Mke wa Rais na Mwenyekiti wa WAMA, Mama Salma Kikwete akifuatana na Mkuu wa Mkoa wa Pwani Injinia Evarist Ndikilo (kulia) na Makamu Mwenyekiti wa WAMA Mheshimiwa Zakhia Meghji (kushoto) wakiingia kwenye ukumbi wa Shule ya Sekondari Nwama-Nakayama kuhudhuria Tamasha la Elimu ya Afya ya Uzazi kwa Vijana wa Shule hiyo tarehe 2.5.2015.
Mke wa Rais na Mwenyekiti wa Taasisi ya WAMA, Mama Salma Kikwete akimkaribisha Mgeni Rasmi Mkuu wa Mkoa wa Pwani Injinia Evarist Ndikilo kutoa hutuba yake wakati wa tamasha la Elimu ya Afya ya Uzazi kwa Vijana lililofanyika kwenye Shule ya Sekondari WAMA-Nakayama na kushirikisha pia Shule za Mahege na Nyamisati.
Mkuu wa Mkoa wa Pwani Injinia Evarist Ndikilo akuwahutubia wakati wa Tamasha la Elimu ya Afya ya Uzazi lililofanyika kwenye Shule ya Sekondari ya WAMA-Nakayama ikizishirikisha pia Shule za Sekondari Mahege na Nyamisati tarehe 2.5.2015.
Baadhi ya wanafunzi na wageni waalikwa wakifuatilia kwa makini hotuba ya Mgeni Rasmi Mkuu wa Mkoa wa Pwani Injinia Evarist Ndikilo kwenye Tamasha la Elimu ya Afya ya Uzazi kwa vijana lililofanyika tarehe 2.5.2015 huko Shule ya Sekondari WAMA-Nakayama iliyoko wilayani Rufiji katika Mkoa wa Pwani.
Baadhi ya walimu wa Shule ya Sekondari ya WAMA-Nakayama wakifuatilia kwa makini tamasha la Elimu ya Afya ya Uzazi kwa Vijana lililofanyika shuleni hapo tarehe 2.5.2015.
Mtoa mada kutoka Wizara ya Elimu na Mafunzo ya Ufundi akieleza umuhimu wa wanafunzi kufundishwa Stadi za Maisha ili wanafunzi wa kike waweze kutimiza ndoto zao za maisha.
Baadhi ya wanafunzi wa Shule ya Sekondari ya WAMA-Nakayama wakionyesha maigizo mbalimbali yanayoweza kumkwamisha mwanafunzi wa kike asifikie malengo yake wakati wa Tamasha la Elimu ya Afya ya Uzazi kwa vijana.
Mke wa Rais Mama Salma Kikwete akijumuika na wanafunzi wa Shule ya Sekondari WAMA-Nakayama kucheza wimbo wa ‘Nani ka Mama’ wakati wa Tamasha la Elimu ya Afya ya Uzazi kwa Vijana lililofanyika Shuleni hapo tarehe 2.5.2015.
No comments:
Post a Comment