Saturday, May 09, 2015

Mfumuko wa bei wa huduma na bidhaa wapanda kwa asilimia 4.5


  Mkurugenzi wa Sensa ya Watu na Takwimu za Jamii wa Ofisi ya Taifa ya Takwimu (NBS), Iphrahim Gwesigabo akizungumza katika mkutano na waandishi wa habari Dar es Salaam leo, kuhusu kupanda kwa mfumuko wa bei wa huduma na bidhaa. Kushoto ni Meneja wa Takwimu za Ajira na Bei, Luth Minja.
Wanahabari wakichukua taarifa hiyo.

Na Dotto Mwaibale
OFISI ya Taifa ya Takwimu imesema mfumuko wa bei umeongezeka kwa asilimia 4.5 kutoka asilimia 4.3 kwa Machi mwaka huu ambapo umeongezeka kwa asilimia 0.8 kutoka asilimia 0.7 Machi,2015.

Ongezeko hilo limechangiwa na kasi ya upandaji bei za bidhaa na huduma kwa mwaka unaoishia Aprili, 2015 kuongezeka ikilinganishwa na kasi iliyokuwepo ya Machi, 2014.

Akizungumza na waandishi wa habari Dar es Salaam leo Mkurugenzi wa sensa ya watu na Takwimu za jamii, Ephraim Kwesigabo alisema farihisi za bei zimeongezeka hadi 157.21 Aprili, 
mwaka huu kutoka 150.50 Aprili mwaka jana.

"Mfumuko wa bei wa bidhaa za vyakula na vinjwaji baridi kwa Machi mwaka huu umeongezeka hadi asilimia 7.1 kutoka asilimia 5.9 Machi mwaka jana, hii imetokana na kuongezeka kwa bei za bidhaa za vyakula kwa kipindi kinachoishia Aprili, 2015," alisema.

Alisema bei za vyakula kama mchele umepanda kwa asilimia 23.3, unga wa mihogo kwa asilimia 8.4, nyama kwa asilimia 4.9, samaki kwa asilimia 5.8 ambapo maharage yamepanda kwa asilimia 6.8 na sukari kwa asilimia 5.6.

Kwegisabo aliongeza kuwa mfumuko huo kwa Aprili, 2015 umeongezeka kwa asilimia 0.8 ukilinganisha na asilimia 0.7 Machi, 2015 ambapo farihisi za bei zimeongezeka hadi 157.21 Aprili, 2015 kutoka 155.88 Machi, 2015.

"Vyakula vilivyochangia kuongezeka kwa farihisi za bei ni pamoja na mchele kwa asilimia 5.8, mahindi kwa asilimia 6.3, unga wa mahindi kwa asilimia 5.0, samaki waliokaushwa kwa asilimia 3.1, ambapo maharage kwa asilimia 2.9, na viazi mviringo kwa asilimia 7.0, mihogo kwa asilimia 6.4 pia viazi mviringo kwa asilimia 4.0," alisema Kwesigabo.

Aidha uwezo wa shilingi 100 kununua bidhaa na huduma imefikia shilingi 63 na senti 61 Aprili, 2015 kutoka Septemba, 2010 ikilinganishwa na shilingi 64 na senti 15 Machi, 2015.

 Alisema mfumuko huo unamwelekeo unaofanana na nchi za Afrika Mashariki ambapo Uganda umeongezeka kwa asilimia 3.60 kutoka asilimia 1.90 Machi, 2015, Kenya umepanda kwa asilimia 7.08 Aprili, 2015 kutoka 6.31 Machi, 2015. 
 (Imeandaliwa na mtandao wa http://www.habarizajamii.com/)

No comments:

WAZIRI MKUU AMWAKILISHA RAIS DKT. SAMIA SULUHU HASSAN UAPISHO WA RAIS WA MSUMBIJI

  Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akisalimiana na Rais wa  zamani wa Msumbiji, Joaquim Chissano katika sherehe za kumwapisha Rais wa Msumbiji...