Tuesday, April 01, 2014

RAIS DKT. SHEIN AMKARIBISHA IKULU YA ZANZIBAR WAZIRI CHIKAWE

PIX 1 (2)Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk. Ali Mohamed Shein (kulia) akimkaribisha ofisini kwake Ikulu mjini Zanzibar, Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Mhe. Mathias Chikawe. Waziri Chikawe alifika ofisini hapo kwa lengo la kujitambulisha kwa Rais huyo baada ya kuteuliwa kuwa Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi. Viongozi hao pia walijadiliana masuala mbalimbali ya kuimarisha ulinzi na usalama wa Tanzania Bara na Visiwani. Katikati ni Naibu Waziri wa wizara hiyo, Pereira Ame Silima. (Picha zote na Felix Mwagara, Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi).
PIX 2 (2)Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk. Ali Mohamed Shein (kulia) akimsikiliza kwa makini, Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Mhe. Mathias Chikawe (katikati) alipokuwa akifafanua jambo wakati wa mazungumzo yao yaliyofanyika Ikulu ya Zanzibar leo.  Waziri Chikawe alifika ofisini hapo kwa lengo la kujitambulisha kwa Rais huyo baada ya kuteuliwa kuwa Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi. Viongozi hao pia walijadiliana masuala mbalimbali ya kuimarisha ulinzi na usalama wa Tanzania Bara na Visiwani. Kushoto ni Naibu Waziri wa wizara hiyo, Pereira Ame Silima.  (Picha zote na Felix Mwagara, Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi).
PIX 3 (2)Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk. Ali Mohamed Shein (watatu kulia) akiwa katika picha ya pamoja na Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Mhe. Mathias Chikawe (watatu kushoto), Naibu Waziri wa wizara hiyo, Pereira Ame Silima (wapili kulia), Mkurugenzi wa Mamlaka ya Vitambulisho vya Taifa (wapili kushoto). Kulia ni Mkurugenzi wa Vitambulisho vya Taifa, Ofisi ya Zanzibar, Vuai Suleiman. Kushoto ni Kamishna wa Jeshi la Polisi Zanzibar, Hamdan Omary Makame. Waziri Chikawe alifika Ikulu ya Zanzibar kwa lengo la kujitambulisha kwa Rais Shein baada ya kuteuliwa kuwa Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi. Viongozi hao pia walijadiliana masuala mbalimbali ya kuimarisha ulinzi na usalama wa Tanzania Bara na Visiwani. Kushoto ni Naibu Waziri wa wizara hiyo, Pereira Ame Silima.  (Picha zote na Felix Mwagara, Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi).
PICHA ZOTE NA KITENGO CHA MAWASILIANO YA SERIKALI
WIZARA YA MAMBO YA NDANI YA NCHI

No comments:

WIZARA YA ARDHI YAPONGEZWA KUTENGA FEDHA KUKAMILISHA MRADI WA MAKTABA

Kamati ya Bunge ya Ardhi, Maliasili na Utalii imeipongeza Wizara ya Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi kwa kutenga fedha kiasi cha Shiling...