Rais Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete na Mke wake Mama Salma akipokewa na ujumbe wa Tanzania unaohudhuria mkutano wa siku mbili baina ya Afrika na Ulaya mara baada ya kuwasili kwenye Hoteli ya Sheraton huko Brussels nchini Ubelgiji akitokea nchini Uingereza tarehe 2.4.2014.
Mke wa Rais Mama Salma Kikwete akisalimiana na Mke wa Rais wa Madagascar Mama Lalao Rajaonarimampianina muda mfupi kabla ya kushiriki kwenye chakula cha mchana kilichoandaliwa na wenza wa mabalozi wa Afrika kwa ajili ya wake wa Marais na Wakuu wa nchi za Afrika wanaohudhuria mkutano wa Afrika na Ulaya unaofanyika huko Brussels tarehe 2-3.4.2014.
Mke wa Rais Mama Salma Kikwete akipokea cheti maalum cha ulezi wa heshima wa Chama cha wenza wa mabalozi wa nchi za Afrika walioko nchini Ubelgiji (Honory Patronese of the Association of the Spouses of African Ambassadors in Belgium) kutoka kwa Mke wa Balozi wa Cameroon nchini Ubelgiji Mama Christiane Eloundov de Evina wakati wa chakula cha mchana walichowaandalia wake wa Marais wa Afrika jijini Brussels tarehe 2.4.2014
No comments:
Post a Comment