Thursday, April 17, 2014

BENKI YA CRDB YAPEWA TUZO KWA KUCHANGIA MAENDELEO YA MKOA WA MOROGORO

Mkuu wa Mkoa wa Morogoro, Joel Bendela kushoto, akimkabidhi  kikombe Mkurugenzi wa Wateja Binafsi na wa kati wa Benki ya CRDB, Nelia Ndosa wakati wa kutoa tuzo zilizotolewa na ULUGURU. Benki hiyo imepata tuzo ya heshima ya Uluguru kutokana na mchango mkubwa uliotolewa na benki hiyo katika kuisaidia jamii ya watu wa Mkoa wa Morogoro. 
Mkurugenzi wa Wateja Binafsi na wa Kati wa Benki ya CRDB, Nelia Ndosa kushoto na Mkurugenzi wa benki hiyo Mkoa wa Morogoro Pendo Issey katikati wakiwa wameshikilia kombe walilokabidhiwa na Mkuu wa Mkoa huo, Joel Bendera hayupo pichani wakati wa utoaji wa tuzo za Heshima za ULUGURU kulia ni mfanyakazi wa benki hiyo.
Wafanyakazi wa Benki ya CRDB Mkoa wa Morogoro wakiwa wameshikilia kombe walilokabidhiwa na Mkuu wa Mkoa huo wakati wa kupokea zawadi  za Heshima  zilizotolewa na ULUGURU AWARD.
 
Mkuu wa Mkoa wa Morogoro, Joel Bendera (katikati), akiwa katika picha ya pamoja na  wafanyakazi wa Benki ya CRDB pamoja na kombe lao.
 
Baadhi ya maofisa wa benki ya CRDB wakiwa katika hafla hiyo.
Wafanyakazi wa Benki ya CRDB Mkoa wa Morogoro wakicheza kwaito wakati wa kupokea zawadi ya Heshima iliyotolewa na ULUGURU AWARD.
Mkurugenzi wa Wateja Binafsi na wa Kati wa Benki ya CRDB, Nelia Ndosa (kushoto), na Mkurugenzi wa benki hiyo Mkoa wa Morogoro, Pendo Issey  katikati wakisalimiana na mteja wa benki hiyo wakati wa kupokea zawadi  ya, ULUGURU AWARD kutokana na benki hiyo kuthamini na kutoa mchango mkubwa kwa wananchi
wa Mkoa huo.
 
Mkurugenzi wa Wateja Binafsi na wa Kati wa Benki ya CRDB, Nelia Ndosa akizungumza na waandishi wa habari.
 Zawadi za vikombe.
 
Mkurugenzi wa Wateja Binafsi na wa Kati wa Benki ya CRDB, Nelia Ndosa kushoto akiwa na Mkurugenzi wa Benki hiyo Mkoa wa Morogoro Pendo Issey.
 Baadhi ya maofisa wa benki ya CRDB wakiwa katika hafla hiyo.

No comments:

WIZARA YA ARDHI YAPONGEZWA KUTENGA FEDHA KUKAMILISHA MRADI WA MAKTABA

Kamati ya Bunge ya Ardhi, Maliasili na Utalii imeipongeza Wizara ya Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi kwa kutenga fedha kiasi cha Shiling...