Mkurugenzi wa Idara ya Habari Maelezo ambaye pia ni Msemaji wa Serikali Assah Mwambene akitolea ufafanuzi juu ya Taarifa iliyotolewa na Gazeti la Mawio mapema jana jijini Dar es Salaam,kushoto ni Afisa habari wa Idara ya Habari -MAELEZO Fatma Salum
---
Serikali imeagiza gazeti la Mawio kueleza sababu za kupotosha na kukejeli nia njema ya serikali kwa wananchi wake kuhusu Hati ya Muungano.
Akizungumza jana, Mkurugenzi Idara ya Habari (MAELEZO), Assah Mwambene alisema
gazeti hilo la wiki linatakiwa kujieleza ndani ya siku tatu.
gazeti hilo la wiki linatakiwa kujieleza ndani ya siku tatu.
Alisema mbali na kujieleza, gazeti hilo limepewa siku saba hadi Aprili 23, mwaka huu, kukanusha taarifa hiyo.
Kwa mujibu wa Mwambene, katika gazeti hilo toleo na 0091 la Aprili 17-23, mwaka huu lenye kichwa cha habari ‘Hati za Muungano utata’, taarifa husika inakebehi hati hiyo na kujenga taswira kwamba ni ya kughushi na batili.
Linadai waandishi wawili ndiyo waliona kati ya waandishi zaidi ya 20 waliokuwepo kwenye mkutano wa Katibu Kiongozi, Balozi Ombeni Sefue.
"Taarifa ya gazeti la Mawio ni ya kimawazona imeandikwa pasipo shaka kutimiza malengo na maslahi binafsi wanayojua,”alisema.
Alisema pamoja na maelezo ya Katibu Kiongozi, Sefue, gazeti hilo liliamua kwa utashi wake kukejeli na kuuaminisha umma wa Watanzana kwamba Hati ya Muungano ina utata.
No comments:
Post a Comment