Thursday, April 17, 2014

MAKAMU WA RAIS ATEMBELEA BANDA LA BODI YA MIKOPO KATIKA MAONESHO YA MIAKA 50 YA MUUNGANO

 Makamu wa Rais Dk. Mohamed Gharib Bilali ametembelea viwanja vya Mnazi Mmoja jijini Dar es Salaam kujionea maonesho ya Miaka 50 ya Muungano yanayoendelea katika vuiwanja hivyo. Miongoni mwa mabanda aliyotembelea ni banda la Bodi ya Mikopo ya Wanafunzi wa Elimu ya Juu (HESLB) na pichani ni Makamu wa Rais akikaribishwa bandano hapo na Kaimu Mkurugenzi Mtendaji wa HESLB, Asangye Bangu.
 Makamu wa Rais Dk. Mohamed Gharib Bilali akisalimiana na watumishi wa HESLB mara baada ya kufika bandani haopo na kupokea maelezo ya shughuli za HESLB ikiwa ni mafanikio, matarajio na changamoto mbalimbali zinazowakabili na jinsi wanavyo jitahidi kukabiliana nazo.
 Kulia ni Kaimu Mkurugenzi Mtendaji wa HESLB, Asangye Bangu akitoa maelezo kwa Makamu wa Rais, Dk. Mohamed  Gharib Bilali juu ya shughuli za bodi wakati alipotembelea banda la Bodi ya Mikopo ya Wanafunzi wa Elimu ya Juu  (HESLB) lililopo katika viwanja vya Mnazi mmoja yanapofanyika maonesho ya Miaka 50 ya Muuungano Dar es Salaam.
 Makamu wa Rais, Dk. Mohamed Gharib Bilali akitoa neno wakati alipotembelea banda hilo.
Baadhi ya watumishi wa Bodi ya Mikopo wakiwa bandani hapo kusubiri wananchi wawape maelezo ya shughuli zao na nini mtu akifanye apate mkopo.

No comments:

WIZARA YA ARDHI YAPONGEZWA KUTENGA FEDHA KUKAMILISHA MRADI WA MAKTABA

Kamati ya Bunge ya Ardhi, Maliasili na Utalii imeipongeza Wizara ya Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi kwa kutenga fedha kiasi cha Shiling...