Thursday, April 17, 2014

Chuo Kikuu cha Bagamoyo chawaasa wahitimu wa kozi ya Utetezi wa Haki za Binadamu

CHUO Kikuu Cha Bagamoyo (UB) Dar es Salaam, kimewataka
wahitimu walioitimu kozi ya utetezi wa Haki za binadamu na Haki za kijamii kutumia taaluma hiyo waliyoipata Katika nchi za Afrika Mashariki bila woga ili waweze Kuwatetea wananchi ambao Haki zao zinapunjwa na hawajui jinsi ya kuzidai.
Rai hiyo imetolewa na Mkuu wa Kitivo Cha Sheria Cha Chuo Kikuu Cha Bagamoyo (UB), Dk.Natujwa Mvungi juzi katika mahafali ya kuwakabidhi jumla ya wahitimu 10 yaliyofanyika Katika Ukumbi wa chuo hicho uliopo KAWE Beach Da es Salaam, ambapo Mafunzo hayo yalifadhiliwa na taasisi ya Akiba Uhaki  Foundation ya nchini Kenya.
Dk.Natujwa ambaye pia ni Mratibu wa kozi hiyo Alisema kozi hiyo Ulianza Septemba Mwaka Jana na kumalizika Machi mwaka huu, ambapo wahitimu kutoka nchini za Afrika Mashariki  wakiwa na fursa ya kafundishwa na Wanasheria toka vyuo
mbalimbali jinsi ya kuweza kuwa watetezi wa Haki za binadamu katika nchi wanazotoka.
“UB imewafundisha jinsi ya kufahamu Haki za binadamu ni zipi?na wa jibu wa binadamu wa serikali na Jamii yake ni upo na Jinsi ya kuzidai Haki hizo….tunaimani mnavyorudi nchini kwenu mtaenda kutumia elimu hii mliyoipata kwa vitendo ili wale ambao hawajafanikiwa Kuipata elimu hiyo waweze kunufaika na elimu mliyoipata” Alisema Dk. Natujwa.
Kwa upande wake Rais wa Chama Cha Tanganyika Law Society(TLS)” Charles Rwechungura, akipongeza UB, na
Taasisi ya Akiba Uhaki KWA kuendesha Mafunzo hayo kutoka Kwa wahitimu Hao wanaogombea nchi za EAC Kwani licha ya swaps mwanga wahitimu Hao w kufahamu Haki za binadamu pia zimeimalisha mahusiano mema, na kuwataka wahitimu hao wakaitumie vyama elimu waliyoipata katika Jamii zinazowazunguka.
Habari imeandikwa na Happines Katabazi
Mkuu wa Maktaba wa Chuo Kikuu cha Bagamoyo, Masawe akizungumza wakati wa hafla ya utoaji vyeti kwa wahitimu wa Kozi ya Utetezi wa Haki za Binadamu na Haki za Kijamii iliyofanyika jijini Dar es Salaam.
 
Mhadhiri wa Chuo Kikuu cha Bagamoyo, Dk. Kasoga akisoma hotuba yake.
Mratibu wa Mafunzo hayo kutoka akibaUhaki, Kepta Ombati akizungumza wakati wa hafla ya kutoa vyeti kwa wahitimu wa Kozi ya Utetezi wa Haki za Binadamu na Haki za kijamii iliyofanyika jijini Dar es Salaam.
Kaimu Ofisa Mtendaji Mkuu wa Chama Cha Wanasheria Tanganyika (TLS), Alphonce Gura akizungumza wakati wa hafla ya kutoa vyeti kwa wahitimu wa kozi ya utetezi wa Haki za binadamu na Haki za kijamii iliyofanyika katika Chuo Kikuu cha Bagamoyo jijini Dar es Salaam.
Mkuu wa Kitivo Cha Sheria Cha Chuo Kikuu Cha Bagamoyo(UB), Dk.Natujwa Mvungi akizungumza wakati wa hafla hiyo.
ProfPalamagamba Kabudi akizungumza na wahitimu wa kozi ya Utetezi wa Haki za binadamu na Haki za kijamii iliyofanyika katika Chuo Kikuu cha Bagamoyo jijini Dar es Salaam.
Gachichi Gachere akipokea cheti kutoka kwa Kaimu Ofisa Mtendaji Mkuu wa Chama Cha Wanasheria Tanganyika (TLS), Alphonce Gura.

No comments:

WIZARA YA ARDHI YAPONGEZWA KUTENGA FEDHA KUKAMILISHA MRADI WA MAKTABA

Kamati ya Bunge ya Ardhi, Maliasili na Utalii imeipongeza Wizara ya Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi kwa kutenga fedha kiasi cha Shiling...