Meya wa Jiji la Mwanza, Stanslaus Mabula akipeperusha bendera jana kuashiria uzinduzi wa upatikanaji wa magazeti ya Mwanachi, Mwanaspoti na The Citizen katika Kanda ya Ziwa. Nyuma yake ni Mjumbe wa Bodi ya MCL, Wangethi Mwangi, Mwenyekiti wa Bodi, Zuhura Muro, Mjumbe wa Bodi, Prof Paramagamba Kabudi na Mkurugenzi Mtendaji, Tido Mhando. Picha na Michael Jamson
---
Kampuni ya Mwananchi Communications Ltd. (MCL), jana ilizindua mpango kabambe wa kuchapisha magazeti yake jijini Mwanza na kuyasambaza asubuhi katika mikoa yote ya Kanda ya Ziwa.
Akizindua uchapishaji wa magazeti ya kampuni hiyo ambayo ni Mwananchi, The Citizen na Mwanaspoti usiku wa kuamkia leo, Meya wa Jiji la Mwanza, Stanslaus Mabula alisema hatua hiyo itawaepusha wasomaji wa maeneo hayo kusoma “habari viporo” walizokuwa wakipata kwa muda mrefu.
Mabula alisema upatikanaji habari kwa wakati kwa njia ya magazeti katika Kanda ya Ziwa umekuwa ni moja ya changamoto kubwa kwa miaka mingi.Kwa habari zaidi Bofya na Endelea.....
No comments:
Post a Comment