Ofisa Uhusiano wa Airtel, Jane Matinde akionyesha simu aina ya Samsung S5 mara baada ya kuzindua ofa itakayowawezesha wateja wake kununua simu hiyo na kujipatia vifurushi vya muda wa maongezi, sms pamoja na data bure.
Kampuni ya simu za mkononi ya Airtel leo imetangaza ofa kabambe inayowawezesha wateja wake kununua simu ya kisasa ya aina Samsung S5 na kupata vifurushi vya muda wa maongezi, sms pamoja na data bure.
Akiongea wakati wa kutangaza ofa hiyo Afisa Uhusiano wa Airtel bi Jane Matinde alisema” leo tunayofuraha kuwatangazia wateja wetu ofa kabambe ambayo inawawezesha kununua simu ya Samsung S5 na kupata dakika 1500 bure.
SMS 5000 kutuma mitandao yote pamoja na kifurushi cha internet cha 3GB kitakachomwenzesha wateja wetu kuperuzi katika mitandao kama vile facebook na twitter kupitia huduma yetu ya internet ya 3.75G yenye kasi zaidi. Vifurushi hizi vitadumu kwa muda wa mwenzi mmoja kuanzia tarehe ambayo mteja atafanya manunuzi ya simu ya Samsaung S5”.
Simu hii ya Samsung S5 inapatikana katika maduka ya Airtel yaliyopo Moroco, Mlimanicity, Jmall pamoja na maduka yote ya Samsung pamoja na maduka yanayouza simu za smart phones yaliyoko nchi nzima.
Tunachukua nafasi hii kuwahimiza watanzania kuwa wakwanza kuchangamkia ofa hii” aliongeza Jane Matinde.
No comments:
Post a Comment