Friday, April 11, 2014

WAZIRI MEMBE AKUTANA NA GAVANA WA JIMBO LA MARYLAND, MAREKANI


Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa, Mhe. Bernard K. Membe (Mb.) akisalimiana na Gavana wa Jimbo la Maryland la nchini Marekani, Mhe. Martin O'Malley walipokutana jijini Washington D.C kwa mazungumzo kuhusu namna ya kuimarisha ushirikiano kati ya Jimbo hilo na Tanzania katika masuala ya uchumi, jamii na siasa. Mhe. Membe alipata fursa ya kukutana na Gavana huyo alipokuwa mjini humo kwa ajili ya kumwakilisha Mhe. Jakaya Mrisho Kikwete, Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kwenye upokeaji Tuzo ya Kiongozi mwenye Mchango Mkubwa zaidi katika Maendeleo ya Bara la Afrika kwa Mwaka 2013. 
Mhe. Gavana O'Malley akisalimiana na Balozi wa Tanzania nchini Marekani, Mhe. Liberata Mulamula

Mhe. Waziri Membe akitoa salamu maalum kwa wajumbe kabla ya mkutano kuanza. Pembeni ni Mhe. Gavana O'Malley. 
Mhe. Membe akizungumza huku Gavana O'Malley akimsikiliza.
Mhe. Membe akiendelea na mazungumzo huku Mhe. Gavana O'Malley na wajumbe wengine wakimsikiliza. 
Mhe. Gavana O'Malley akizungumza.
Balozi Mulamula akiwa na wajumbe wengine wakimsikiliza Gavana O'Malley (hayupo pichani) 
Mkurugenzi wa Mawasiliano Ikulu, Bw. Salvatory Rweyemamu akimsikiliza Gavana O'Malley (hayupo pichani). Wengine ni Balozi wa Nigeria nchini Marekani Prof. Adebowele Adufye pamoja na Bi. Mindi Kasiga, Mkuu wa Kitengo cha Mawasiliano ya Serikali, Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa.
Wajumbe wengine wakati wa mkutano kati ya Mhe. Membe na Gavana O'Malley (hawapo pichani). Kushoto ni Bw. Thobias Makoba, Katibu wa Waziri Membe na Bi. Redemptor Tibaigana, Afisa Mambo ya Nje.
Wajumbe wengine

Mhe. Membe akimweleza jambo Mhe. Gavana O'Malley mara baada ya mazungumzo yao. 
Mhe. Membe akisalimiana na Bw. John Kennedy Opara, Katibu Mtendaji wa Tume ya Mahujaji Wakiristo wa Nigeria ambaye pia ni Mshauri wa Rais Goodluck Jonathan wa nchi hiyo kuhusu Uhusiano wa Kidini nchini Nigeria. Bw. Opara pia alipokea Tuzo ya Heshima siku hiyo.

Mhe. Gavana O'Malley katika picha ya pamoja na Bal. Mulamula
Mhe. Gavana O'Malley katika picha ya pamoja na Bi. Kasiga.
Mhe. Membe na Mhe. Gavana O'Malley katika picha ya pamoja na wajumbe wengine.

No comments:

WIZARA YA ARDHI YAPONGEZWA KUTENGA FEDHA KUKAMILISHA MRADI WA MAKTABA

Kamati ya Bunge ya Ardhi, Maliasili na Utalii imeipongeza Wizara ya Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi kwa kutenga fedha kiasi cha Shiling...