Friday, April 11, 2014

KATIBU MKUU WA CCM, KINANA AKAGUA MPAKA WA TANZANIA NA BURUNDI

Katibu Mkuu wa CCM,Kinana akiwa na viongozi wengene wakiangalia jinsi watanzania wanavyopata taabu na kunusurika kifo kwa kuvuka kwenye Mto Malagalasi wakitokea kuuza bidhaa zao na kununua mahitaji mengine katika Soko Buhinja, Kijiji cha Mrambi, Mkoa wa Makamba nchini Burundi.
Wananchi hao kutoka Kijiji cha Kibande na vijiji viongine wilayani Buhigwe, Kigoma Tanzania, huenda Burundi kufanya biashara kutokana na upande wa Tanzania kutokuwepo na soko kunakosababishwa na kodi…


Katibu Mkuu wa CCM,Kinana akiwa na viongozi wengene wakiangalia jinsi watanzania wanavyopata taabu na kunusurika kifo kwa kuvuka kwenye Mto Malagalasi wakitokea kuuza bidhaa zao na kununua mahitaji mengine katika Soko Buhinja, Kijiji cha Mrambi, Mkoa wa Makamba nchini Burundi.
Wananchi hao kutoka Kijiji cha Kibande na vijiji viongine wilayani Buhigwe, Kigoma Tanzania, huenda Burundi kufanya biashara kutokana na upande wa Tanzania kutokuwepo na soko kunakosababishwa na kodi nyingi.
Katibu Mkuu wa CCM, Abdulrahman Kinana akiangalia mto Malagalasi ambao ni mpaka wa Tanzania na Burundi, alipokuwa katika ziara wilayani Buhigwe mkoani Kigoma,Kinana yupo katika ziara ya siku 5 mkoani humo ya kuimarisha uhai wa chama na kukagua miradi ya maendeleo inayotekelezwa kwa kufuata Ilani ya CCM.
Hizi ni baadhi ya picha zinazoonesha jinsi wananchi wa Tanzania wakivuka mto huo na wengine kuvushwa kwa malipo, wakirudi Tanzania baada ya kufanya biashara upande wa Burundi.
Watu wote hao wakisubiri kuvushwa kwenye mto huo Malagalasi,kwa kimtumbwi kimoja ama kubebwa kama baadhi ya picha zinavyoonyesha Baadhi ya Wanahabari pichani Kulia Bakari Kimwanga kutoka gazeti la Mtanzania na Bwana Jongo kutoka gazeti la Uhuru wakionja joto ya kuvushwa kwenye mto wa Malagalasi ambao ndio sehemu ya mpaka kati ya Burundi na Tanzania.
Kuonja adha hiyo hulipia kiasi cha fedha shilingi 500 mpaka 1000 kama nauli. Katibu Mkuu wa CCM,Ndugu Kinana akizungumza jambo kwa msisitizo na Mkurugenzi wa Maendeleo wa Halmashauri ya Buhigwe,Kaondo Julius walipokwenda kukagua mpaka wa Tanzania na Burundi alipokuwa katika ziara wilayani Buhigwe mkoani Kigoma.
Msanii wa kikundi cha ngoma za utamaduni kutoka Burundi wakitumbuiza katika mkutano wa hadhara uliofanyika Uwanja wa Kibande, Wilaya ya Buhigwe mkoani Kigoma. Katibu Mkuu wa CCM,Ndugu Kinana akisalimiana na Makamu Mwenyekiti wa chama cha CNDD-FDD,Mkoa wa Makamba nchini Burundi,Bwa.
Nishimwe Zen,kabla ya mkutano wa hadhara kufanyika katika kijiji cha Kibande,wilayani Buhigwe mkoani Kigoma.

No comments:

WIZARA YA ARDHI YAPONGEZWA KUTENGA FEDHA KUKAMILISHA MRADI WA MAKTABA

Kamati ya Bunge ya Ardhi, Maliasili na Utalii imeipongeza Wizara ya Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi kwa kutenga fedha kiasi cha Shiling...