Mgombea ubunge wa Jimbo la Chalinze Ridhiwan Kikwete, akizungumza na waandishi wa habari mara baada ya kutangazwa matokeo ya uchaguzi huo yaliyotangazwa usiku wa kuamkia leo,. ambapo Mgombea huyo ameibuka na ushindi wa kishindo kwa jumla ya kura 20, 000 kati ya 24, 000, zilizopigwa katika uchaguzi huo jana.
--
MATOKEO RASMI JIMBO LA CHALINZE;
Hatimaye Ridhiwani Kikwete aibuka kidedea ubunge Chalinze kwa 86.61% akiwa amepigiwa kura na wakazi 20,828,matokeo yametangazwa saa9 usiku wa jana.
Mathayo Torongei ameshika nafasi ya pili na alipata kura 2,544 sawa na 10.58%,huku Mgombea wa CUF Bw.Fbian Skauki akishika nafasi ya tatu akiwa na kura 476 sawa na 1.98%,Chama cha AFP kikishika nafasi ya nne kupitia mgombea wake Ramadhani Mgaya akiwa na kura 186 sawa na 0.59% na nafasi ya mwisho ni ya Hussein Ramadhani kupitia chama cha NRA aliyepata kura 60 sawa na 0.25% huku kura 375 zikiharibika.
Waliojiandikisha katika daftari la kudumu la wapiga kura ni wakazi elfu 92,waliopiga kura ni watu 24,422 idadi inayotajwa kushuka toka katika uchaguzi uliopita wa mwaka 2010 ambapo wapiga kura katika jimbo hilo walikuwa zaidi ya elfu 36.
Mgawanyo wa kura zilizovyoripotiwa katika Kata:
Talawanda: CCM (1,192), CHADEMA (104), CUF (4)
Msoga: CCM (1,248), CHADEMA (68), CUF (9)
Lugoba: CCM (1,594), CHADEMA (174), CUF (4)
Kiwangwa: CCM (1,180), CHADEMA (80), CUF (14)
Kibindu: CCM (1,131), CHADEMA (300), CUF (3)
Fukayosi: CCM (1,105), CHADEMA (69), CUF (17)
Mandela: CCM (1,394), CHADEMA (112), CUF (8)
Mbwewe: CCM (1,319), CHADEMA (166), CUF (23)
Pera: CCM (1,139), CHADEMA (49), CUF (19)
No comments:
Post a Comment