Taarifa iliyotolewa asubuhi ya leo na mtoto wa kwanza wa Marehemu Mzee Gurumo Ndg Abdallah Gurumo amesema kuwa leo saa 10 jioni kutakuwa na kisomo nyumbani kwa Marehemu eneo la Tabata Kisukulu ambapo Watanzania wote wanakaribishwa.
Baada ya kisomo saa 3 ya asubuhi kesho April 15 mwili wa Marehemu utafikishwa nyumbani kwa ajili ya swala kisha saa 4 asubuhi safari ya kuelekea kijiji cha Masaki wilaya ya Kisarawe Mkoa wa Pwani itaanza kwa ajili ya maziko ya Mzee Gurumo.
Kwa mtu asiyepafamu nyumbani kwa Mzee Gurumo ukiwa unatokea Ubungo kabla ya Mwananchi kuna kituo kinaitwa Garage shukia hapo kisha ulizia mtu yoyote atakuelekeza pia kwa wewe unaetokea Tabata, Buguruni au Tazara shukia hapo Garage kituo baada ya Mwananchi.
No comments:
Post a Comment