Tuesday, April 08, 2014

UNHCR YATOA MSAADA WA GARI MPYA KWA IDARA YA WAKIMBIZI, WAZIRI WA MAMBO YA NDANI YA NCHI, MHE. MATHIAS CHIKAWE AIPOKEA

 Kaimu Mkurugenzi wa Idara ya Wakimbizi nchini, Harrison Mseke akilionesha gari ambalo amekabidhiwa na Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Mathias Chikawe baada ya kukabidhiwa na Mwakilishi Mkazi wa Shirika la Umoja wa Mataifa la Kuhudumia Wakimbizi Duniani (UNHCR), Joyce Mends-Cole. Gari hiyo imetolewa na Shirika hilo kwa ajili ya kusaidia shughuli mbalimbali za kiutendaji zifanywazo na Idara ya Wakimbizi nchini iliyopo ndani ya Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi. Tukio la makabidhiano hayo lilifanyika katika ofisi za wizara hiyo, jijini Dar es Salaam leo. .
 Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Mathias Chikawe (kushoto) akipokea ufungua wa gari kutoka kwa Mwakilishi Mkazi wa Shirika la Umoja wa Mataifa la Kuhudumia Wakimbizi Duniani (UNHCR), Joyce Mends-Cole. Gari hiyo ambayo ni mpya aina ya Toyota Land Cruiser imetolewa na Shirika hilo kwa ajili ya kusaidia shughuli mbalimbali za kiutendaji zifanywazo na Idara ya Wakimbizi nchini iliyopo ndani ya Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi. Tukio la makabidhiano hayo lilifanyika katika ofisi za wizara hiyo, jijini Dar es Salaam

Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Mathias Chikawe (kulia) akiifurahia gari mpya aina ya Toyota Land Cruiser baada ya kukabidhiwa na Mwakilishi Mkazi wa Shirika la Umoja wa Mataifa la Kuhudumia Wakimbizi Duniani (UNHCR), Joyce Mends-Cole (kushoto). Gari hiyo imetolewa na Shirika hilo kwa ajili ya kusaidia shughuli mbalimbali za kiutendaji zifanywazo na Idara ya Wakimbizi nchini iliyopo ndani ya Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi. Tukio la makabidhiano hayo lilifanyika katika ofisi za wizara hiyo, jijini Dar es Salaam .Picha na Felix Mwagara, Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi.

No comments:

WIZARA YA ARDHI YAPONGEZWA KUTENGA FEDHA KUKAMILISHA MRADI WA MAKTABA

Kamati ya Bunge ya Ardhi, Maliasili na Utalii imeipongeza Wizara ya Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi kwa kutenga fedha kiasi cha Shiling...