Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akiweka jiwe la msingi la ujenzi wa nyumba 60 za makazi ya watu zinazojengwa na Shirika la Nyumba ya Taifa katika Wilaya ya Mlele mkoani Katavi.
Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akipata maelezo kutoka kwa Meneja wa Shirika la Nyumba Mkoa wa Katavi Ndugu Nehemia Msigwa juu ya miradi ya ujenzi wa nyumba itakayofanyika ndani ya mkoa wa Katavi.
Pichani
ni Michoro ya Nyumba zitakazojengwa mkoani Katavi na Shirika la Nyumba
ya Taifa,ambapo wilaya ya Mlele ,Shirika la Nyumba linajenga nyumba 60
na zitachukua miezi nane kukamilika.
Mkuu wa Mkoa wa Katavi Dr. Rajab Rutengwe akizungumza mbele ya Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana wakati wa uwekaji wa jiwe la msingi la uzinduzi wa nyumba 60 zitakazojengwa na Shirika la Nyumba la Taifa katika wilaya ya Mlele.
Meneja wa Huduma za Jamii wa Shirika la Nyumba la Taifa Ndugu Muungano Saguya akizungumzia namna Shirika la Nyumba lilivyojipanga katika kuboresha makazi ya watu katika mkoa wa Katavi.
Picha na Adam Mzee
Shirika la Nyumba Mkoa wa Katavi/Rukwa umejizatiti katika kutekeleza mpango Mkakati wa Shirika wa miaka mitano yaani 2010/2011 hadi 2014/2015 kama ilivyokwa mikoa mingine katika Shirika la Nyumba la Taifa. Mpango huu umekuja wakati mwafaka kushughulikia tatizo la uhaba wa nyumba za makazi na biashara kwa Mkoa huu wa Katavi/Rukwa. Katika Mpango Mkakati huu, Shirika limejiwekea Dira, Dhima, Maadili ya Msingi, Malengo na Matarajio ya Shirika.
Wakati Utekelezaji wa Mpango huu unaendelea kwa sasa, unasaidia sana katika kukuza uchumi kwa katika mkoa wetu kwa njia ya kuongeza Ajira mbalimbali pamoja na kodi, na hili linatokana na uwezo mkubwa wa sekta ya Nyumba katika kukuza uchumi katika eneo husika. Zaidi sana ni Msisitizo wetu NHC-Katavi/Rukwa kuwa, Maendeleo ya Mikoa hii, lazima yaendane na Ujenzi wa Nyumba Bora za Makazi na za Biashara. Na kwa hili NHC tunaelekea kukamilisha malengo yetu mawili ya kuwa Kiongozi Mahiri katika Kuendeleza Milki na Pia kuwa Msimamizi Mahiri wa Miliki si hapa Katavi tu bali Tanzania Nzima.
Kwa sasa kuna miradi Mitano ambayo ipo katika hatua mbalimbali ambayo inatekelezwa na Shirika katikakufikia malengo shirika tuliyojiwekea.
Kuna Mradi wa Ilembo ambao unatarajiwa kukamilika 30/Mei/2014. Mradi huu una jumla ya nyumba 90. Ni mradi mkubwa kwa eneo kama la Mpanda ambao utakuwa name gharama ya said I ya Tsh. 3.1 Bil. kuwepo na umesaidia sana kutia hamasa kwa wananchi wa Mpanda kuongeza kasi katika sekta ya ujenzi wa Nyumba, pia umesaidia kuleta mandhari bora ya makazi. Ni matarajio yetu, kwa kuwa tumeshaanza kuuza nyumba hizo, Taasisi za Serikali, Mashirika ya Umma, Mashirika Binafsi, Halmashauri za Miji ambazo katika mkoa wa katavi watumishi wake wengi wanakosa Nyumba bora za kuishi watazichangamkia Nyumba hizi kwa kuzinunua na kuwapangiza watumishi wake. Vilevile ni matarajio yetu kuwa Wananchi nao kila mmoja binasfi watajitokeza kwa wingi kununua Nyumba hizi ambazo ni Bora kwa makazi.
Katika Wilaya Mpya ya Mlele, Mradi wa nyumba za Gharama nafuu upo katika hatua za awali, ni mmatarajio yetu mara baada kukamilika kwa Mradi huo tatizo la uhaba wa nyumba Bora za Kuishi pale Inyonga, ambapo ndipo makao makuu ya Wilaya, litakuwa limedhibitiwa kwa kiasi kikubwa, rai yetu ni ileile kwa taasisi za serikali, Mashirika ya Umma, pamoja na Mashirika Binasfi zichangamkie fursa hiyo ya kupata nyumba kwa ajili ya Watumishi wake.
Miradi kama hii ya Ilembo-Mpanda pamoja na Inyonga tunatarajia pia kuipeleka katika Wilaya za Kalambo pamoja na Nkasi mkoa wa Rukwa na Halmashauri ya Nsimbo mkoani Katavi. Miradi katika wilaya hizi itaanza mara tu taratibu husika zitakapo kamilika. Ninatoa Ari kuwa halmashauri ambazo zitatoa ushirikiano chanya kwa NHC katika kutatua tatizo hili la uhaba wa nyumba bora za makazi kwa wafanyakazi wake na wananchi kwa ujumla ndio itakayofikiriwa zaidi, hii ni pamoja na changamoto za bei kubwa za Viwanja tunazokumbana nazo kutoka kwa halmashauri husika.
Katika orodha ya Miradi ambayo ipo katika Mkoa huu ni pamoja na Mradi wa Jengo la Biashara litajengwa katika eneo la Paradise-Mpanda hapa Mkoani Katavi na Mradi wa Nyumba za Makazi katika eneo la Jangwani-Sumbawanga Mkoani Rukwa. Miradi hiyo yote imeshatangazwa kwa ajili ya Kupata wakandarasi watakao jenga miradi hiyo, hivyo muda si mrefu miradi hiyo itaanza rasmi.
Katika hatua nyingine, ili kutatua tatizo la uhaba wa kumbi za mikutano, Shirika la Nyumba la Taifa kwa kushirikiana na Halmashauri ya Mji ya Mpanda watajenga Ukumbi wa Kisasa wa Mikutano katika eneo la madini (Madini Plot). Huu ni mradi mwingine katika Mji wa Mpanda ambao si tu utaleta mandhari nzuri kwa Mkoa wa Katavi bali pia Utafanya Mkoa wa Katavi kuwa Kitovu cha mikutano muhimu ya Ushirikiano kwa mikoa ya kanda hii ya ziwa Tanganyika na Nchi jirani, hivyo pia kuchangai ukuaji wa uchumi katika mkoa huu.
Napenda pia kuchukua fursa hii kuzishauri Halmashauri za Miji taasisi za serikali, mashirika ya umma yote yanao jiusisha na utoaji wa huduma za miundo mbinu (Maji, Umeme pamoja na Barabara) kuwa sisi NHC ni wabia wao wakubwa kwani tunachangia kwa kiasi kikubwa kuwatafutia wateja wapya katika kila Mradi husika. Hivyo pindi tunapoanza ama hata kabla ta kuanza mradi husika huduma zao zinahitajika.
MPANGO WA SHIRIKA LA NYUMBA WA KUSAIDIA VIJANA KWENYE HALMASHAURI ZA WILAYA NA MIJI MASHINE ZA KUFYATULIA MATOFALI
Katika kuunga mkono jitihada za dhati zinazofanywa na Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, kuongeza ajira za vijana na kupunguza umaskini hapa nchini na hasa Mikoa ya Katavi na Rukwa, Shirika limeamua kutoa mashine za kufyatulia matofali kwa Halmashauri zote zilizoko katika Mikoa hii, zikiwemo Halmashauri za Mlele, Nsimbo, Mpanda Mji pamoja na Halmashauri ya Mpanda Vijijini kwa Mkoa wa Katavi, Pia Halmashauri Manispaa ya Sumbawanga, Halmashauri ya Wilaya ya Nkasi-Namanyere Pamoja na Halmashauri ya Wilaya ya Kalambo katika Mkoa wa Rukwa.
Mashine hizo zitatumiwa na vikundi vya vijana vitakavyoundwa na Halmashauri kwa kushirikiana na Meneja wa Mikoa wa NHC. Kila kikundi cha vijana kitapewa msaada wa mashine nne (4) ambazo, kila mashine itakuwa ikihudumia vijana wapatao 10 hivyo vijana 40 katika kila Halmashauri. Pamoja na msaada wa mashine, Shirika litatoa Shilingi laki tano (500,000/=) kwa kila kikundi kama kianzio cha vijana hao kununua vifaa muhimu vya kuwezesha kazi ya kufyatua matofali kuanza. Aidha, vikundi hivyo vya vijana vitaweza baadae kuunda SACCOS zao na hivyo kupanua shughuli zao za kiuchumi.
Ili kufanikisha mpango huo, Shirika kwa kushirikiana na Wakala wa Utafiti wa Vifaa Bora vya Ujenzi wa Nyumba (NHBRA) iliyo chini ya Wizara ya Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi, pamoja na Mamlaka ya Elimu na Ufundi Stadi (VETA) litatoa mafunzo ya siku 21 kati ya mwezi Desemba 2013 na Januari 2014 kwa wakufunzi wapatao 50, ya namna ya kutumia mashine hizo. Wataalam hawa ndio watakaotumika katika kuvifundisha vikundi vya vijana katika Halmashauri kuanzia mwezi Januari hadi Juni 2014.
Shirika la Nyumba la Taifa linatanguliza Shukrani kwa kutuunga mkono katika kufanikisha jambo hili muhimu kwa maendeleo ya nchi yetu.
“KATAVI BILA UMASIKINI INAWEZEKANA, KWA KUWA MAISHA NI NYUMBA”
MAISHA YANGU NYUMBA YANGU
IMETOLEWA NA
NEHEMIA L. MSIGWA
MENEJA WA MKOA
SHIRIKA LA NYUMBA LA TAIFA
No comments:
Post a Comment