Wednesday, April 30, 2014

Mkurugenzi wa Idara ya Habari (MAELEZO), Assah Mwambene amesema Jaji Joseph Warioba alitunukiwa tuzo ya muungano iliyotukuka kwa kuwa alistahili kupewa kama viongozi wengine na kuwa kitendo si kumkejeli kama baadhi ya vyombo vya habari vilivyoripoti hivi karibuni.

Mkurugenzi Idara ya Habari Assah Mwambene akitoa ufafanuzi mbele ya  Waandishi wa Habari (hawapo pichani) juu ya tuzo aliyopewa Jaji Joseph Sinde Warioba wakati wa Sherehe za Muungano, ufafanuzi huo umetolewa leo katika Ukumbi wa Idara ya Habari Maelezo jijini Dar es Salaam.
Mkurugenzi Idara ya Habari Assah Mwambene (kushoto) akijibu maswali mbalimbali wakati wa Mkutano na Waandishi wa Habari (hawapo pichani) juu ya tuzo aliyopewa Jaji Joseph Sinde Warioba wakati wa Sherehe za Muungano. Kulia ni Mkurugenzi Msaidizi Vicent Tiganya. Mkutano huo umefanyika leo katika Ukumbi wa Idara ya Habari Maelezo jijini Dar es Salaam.
read more

Soma Taarifa ya Mamlaka ya Udhibiti wa Huduma za Nishati na Maji (EWURA) ya Kufuta Leseni za kufanya biashara ya mafuta kwa jumla (Whole Sale Licenses) kwa Kampuni tisa (9) zinazojihusisha na biashara hiyo hapa nchini.


BODI ya Wakurugenzi ya Mamlaka ya Udhibiti wa Huduma za Nishati na Maji (EWURA) imefuta leseni za kufanya biashara ya mafuta kwa jumla (Whole Sale Licenses) kwa Kampuni tisa (9) zinazojihusisha na biashara hiyo hapa nchini.


Uamzi huo umefanywa leo (29.4.204) katika kikao chache cha Bodi ya Wakurugenzi kilichoongozwa na Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi wa EWURA, Bw. Simon Sayore kutokana na kampuni hizo kukiuka masharti ya biashara.


Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa na Mkurugenzi Mkuu wa EWURA, Bw. Felix Ngamlagosi, kufutwa kwa
leseni hizo kumetokana na ukikaji kwa sheria na kanuni za biashara hiyo.


Bw. Ngamlagosi katika taarifa yake, alisema kampuni hizo zimefutiwa leseni kutokana na kukaa bila kuagiza mafuta kama leseni inavyowataka kwa kipindi cha zaidi ya miezi sita tangu kupewa leseni hizo na EWURA.

Kampuni zilizofutiwa leseni ni pamoja na Aspam Energy (T) Limited, MPS Oil Tanzania Limited, Panone Bulk Oil Importers Limited, Petcom (T) Limited, KMJ Tanzania Limited, Horizon Petroleum Company Limited, G.M and Company (T) Limited na Petronas Energy Tanzania Limited.



Mamlaka ya Udhibiti wa Huduma za Nishati na Maji (EWURA) imeundwa chini ya sheria ya EWURA, sura namba 414 ya Sheria za Tanzania. EWURA ina majukumu ya kusimamia shughuli za udhibiti, kiufundi na kiuchumi katika sekta Nne (4) za Petroli, Umeme, Gasi Asili na Maji Safi na Maji Taka.

IMETOLEWA NA

BW. FELIX NGAMLAGOSI

MKURUGENZI MKUU

EWURA

Waziri wa nishati na madini Mheshimiwa Prof. Sospeter Mwijarubi Muhongo ameteua wajumbe wa Bodi ya Wakurugenzi ya Wakala wa Nishati Vijijini (REA) kutoka Taasisi zisizo za kiserikali (NGO), Sekta Binafsi na washiriki wa Maendeleo kwa kipindi cha miaka mitatu kuanzia tarehe 1 Aprili, 2014 kama ifwatavyo:-

JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA
WIZARA YA NISHATI NA MADINI
Waziri wa nishati na madini Mheshimiwa Prof. Sospeter Mwijarubi Muhongo (Mb) ameteua wajumbe wa Bodi ya Wakurugenzi ya Wakala wa Nishati Vijijini (REA) kutoka Taasisi zisizo za kiserikali (NGO), Sekta Binafsi na washiriki wa Maendeleo kwa kipindi cha miaka mitatu kuanzia tarehe 1 Aprili, 2014.

Majina ya wajumbe walioteuliwa na Taasisi wanazoziwakilisha ni kama ifuatavyo:- Bw. Edmund P. Mkwawa
        Tanzania Banker’s
        Association
ii
Bi Rehema Tukai
        Foundation for Civil
        Society
iii
Bi  Renatha J. Mwageni
        Tanzania Federation
        of Cooperation
iv
Bw. Innocent G. Luoga
        Wizara ya Nishati na
        Madini
 v
Bw. Kalist Luanda
        Ofisi ya Waziri Mkuu –
        TAMISEMI
vi
Bw. Emmanuel M. Tutuba
        Wizara ya Fedha
vii
Dkt Gideon H. Kaunda
        Tanzania Private Sector
        Foundation
vii
Bi Stella Mandago (Observer)
        African Development
        Bank (AfDB)


Wakala wa Nishati Vijijini ulipitishwa kwa Sheria ya Bunge Na. 8 ya mwaka 2005 na uteuzi wa wajumbe hawa umezingatia Sifa muhimu zinazotakiwa kwa wajumbe wa Bodi. Kutokana na kukidhi sifa husika MheshimiwaProf. Sospeter M. Muhongo (Mb) amemteua Bw. Edmund P. Mkwawa kuwa Mwenyekiti wa Wakurugenzi wa Bodi ya Nishati Vijijini

Imetolewa na:

KATIBU MKUU
WIZARA YA NISHATI NA MADINI

Serikali kupitia Wizara ya Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo imemaliza kupitia Rasimu ya Katiba ya Club ya Simba

 Mkurugenzi wa Idara ya Maendeleo ya Michezo  Bw. Leornad Thadeo akiwaonyesha Waandishi wa  Habari Rasimu ya Katiba ya Timu ya Mpira wa Miguu ya Simba baada ya wanahabari kutaka kupata ufafanuzi juu ya hatma ya Katiba na uchaguzi wa Klabu hiyo
Mkurugenzi wa Idara ya Maendeleo ya Michezo Bw. Leornad Thadeo akitoa ufafanuzi kwa Wanahabari hawapo pichani kuhusu Rasimu ya Katiba ya Timu ya Mpira wa Miguu ya Simba baada ya wanahabari kutaka kupata ufafanuzi juu ya hatma ya Katiba na uchaguzi wa Klabu hiyo.Picha na Benjamin Sawe wa WHVUM
---
Na: Genofeva Matemu – Afisa Mawasiliano Serikalini (WHVUM)
Serikali kupitia Wizara ya Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo imemaliza kupitia Rasimu ya Katiba ya Club ya Simba kwa ajili ya kuidhinisha katiba hiyo na kuifanya Club ya Simba kuendelea na taratibu za uchaguzi mkuu.

Mabadiliko ya Anuani ya Ofisi ya Rais,Menejimenti ya Utumishi wa Umma


JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA
 OFISI YA RAIS, MENEJIMENTI YA UTUMISHI WA UMMA
Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma inapenda kuwafahamisha wadau wake kuwa anuani yake imebadilika hivyo kuanzia sasa mawasiliano yafanyike kwa kutumia anuani ifuatayo; 
OFISI YA RAIS, MENEJIMENTI YA UTUMISHI WA UMMA
UTUMISHI HOUSE
8 BARABARA YA KIVUKONI
11404 DAR ES SALAAM
 
au
 
PRESIDENT’S OFFICE, PUBLIC SERVICE MANAGEMENT
UTUMISHI HOUSE
8 KIVUKONI ROAD
11404 DAR ES SALAAM
 
Anuani hii inachukua nafasi ya Sanduku la Posta 2483, Dar es salaam. Hivyo, mawasiliano yote yazingatie anuani mpya.
 
Limetolewa na
Katibu Mkuu
Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma
Barua pepe: permsec@utumishi.go.tz

ASASI YA IRaWS - TANZANIA YAWASILISHA STADI JUU YA JINSI YA KUDHIBITI IDADI YA WAFUNGWA MAGEREZANI LEO

 

  Kamishna wa Huduma za Urekebishaji wa Magereza, Deonice Chamulesile akisoma risala ya ufunguzi katika Kikao cha uwasilishaji wa Stadi juu ya jinsi ya kudhibiti idadi ya Wafungwa Magerezani iliyofanywa na Asasi ya Kiraia ya IRaWS - T. Kikao hicho kimefanyika leo Aprili 30, 2014 katika Ukumbi wa Luther House, Jijini Dar es Salaam(wa kwanza kulia) ni Kamishna Mkuu Mstaafu wa Magereza, Nicas Banzi(wa pili kushoto) ni Kamishna Mkuu Mstaafu wa Magereza Onel Malisa(wa kwanza kushoto) ni Katibu Mtendaji wa Asasi ya IRaWS - T, Naibu Kamishna Mstaafu wa Magereza, John Nyoka.
  Mhadhiri toka Kitivo cha Sheria, Chuo Kikuu cha Dar es Salaam, Bw. James Jesey(aliyesimama) akiwasilisha rasmi Stadi ya jinsi ya kudhibiti idadi ya Wafungwa Magerezani.

Tuesday, April 29, 2014

AIRTEL YAZINDUA WHATSAPP, FACEBOOK NA TWITTER BURE KUPITIA VIFURUSHI VYA YATOSHA

???????????????????????????????Meneja Masoko wa Airtel akionyesha kipeperushi wakati wa uzinduzi wa huduma mpya itakayowawezesha wateja wa Airtel kupata whatsapp, Facebook na Twitter bure kupitia Vifurushi vya yatosha
…………………………………………………………………………………..
Yatangaza facebook, whatsapp and twitter BURE
·       Sasa wateja kupatawhatsapp, Facebook na Twitter bure kupitia yatosha bando
  Kampuni ya simu za mkononi ya Airtel inayoongoza kwa kutoa huduma bora imezindua huduma ya kibunifu itakayowawezesha wateja wake kupata na kuunganishwa kwenye mitandao ya kijamii ya Facebook, Whatsapp na twitter BURE kupitia huduma ya Airtel yatosha 
Akiongelea kuhusu huduma hiyo Mkuu wa kitengo cha mawasiliano wa Airtel Bi Beatrice Singano Mallya alisema” sasa ni bure kabisa kwa wateja wetu wote wa Airtel kuunganishwa na mitandao ya kijamii ya Whatsapp, Facebook na Twitter. Airtel tunayofuraha kutoa nafasi kwa wateja wetu kuwasiliana na marafiki na familia kupitia mitandao hii ya kijamii bure bila makato yoyote, huku tukiendelea kuthibitisha kuwa Airtel Yatosha ni BABA LAO!” 
Aliongeza kwa kusema mteja yoyote atakayenunua kifurushi cha data cha yatosha kuanzia sasa iwe ni cha siku, Wiki au Mwezi vifurushi vyao vya internet vya MB au GB  hazitakatwa katika matumizi ya Facebook, Whatsapp na Twitter na badala yake wataweza kutumia vifurushi vyao vya data kwenye kuperuzi katika mitandao mingine kama vile YouTube na mingine mingi kadri ya mahitaji yao” 
Akiongea kuhusu namna ya kujiunga Meneja Masoko wa Airtel Bi Upendo Nkini alisema” ili kupata Whatsapp, Facebook na Twitter BURE wateja watatakiwa kupiga *149*99# kisha kuchagua kifurushi kinachowafaa na kuanza kufurahia BURE Whatsapp, Facebook na  Twitter” 
“Sambamba na hilo katika kuendeleza ubunifu na kurahisiaha upatikanaji wa vifurushi vya Yatosha,  tumewawezesha wateja wetu  kutumia simu za kununua vifurushi vya yatosha kwa ajili ya marafiki zao familia na kubaki wakiwa wameunganishwa na kufurahia mitandao hii ya kijamii ya Whatsapp, Facebook na  Twitter BURE, furahia kuunganishwa katika mawasiliano kupitia mtandao wa Airtel” aliongeza Nkini

MAMA KIKWETE AZINDUA CHANJO YA KUZUIA MAAMBUKIZO YA SARATANI YA SHINGO YA KIZAZI KWA WASICHANA WENYE UMRI WA MIAKA 9 HADI 16. HUKO MOSHI.

IMG_0089Mkuu wa Mkoa wa Kilimanjaro Ndugu Leonidas Gama akimpokea Mke wa Rais Mama Salma Kikwete kwenye Uwanja wa ndege wa Kimataifa wa Kilimanjaro tarehe 28.4.2014. Mama Salma alikwenda Moshi kuzindua rasmi chanjo ya kuzuia maambukizi ya saratani ya shingo ya kizazi kwa wasichana wa umri wa miaka 9 hadi 16.IMG_0127Mke wa Rais na Mwenyekiti wa Taasisi ya Wanawake na Maendeleo, Mama Salma Kikwete akisalimiana na Mwakilishi wa Shirika la kuhudumia watoto, UNICEF, hapa nchini Dkt. Sudha Sharma, mara baada ya kuwasili kwenye uwanja wa Mandela uliopo katika eneo la Pasua katika Manispaa ya Moshi kwa kulikofanyika uzinduzi rasmi ya chanjo ya saratani ya shingo ya kizazi kwa wasichana.IMG_0147Mke wa Rais Mama Salma Kikwete akiangalia ngoma na vikundi vya kwaya vilivyokuwa vikitumbuiza wakati wa sharehe za uzinduzi wa chanjo ya kuzuia saratani ya shingo ya kizazi kwa wasichana wenye umri wa miaka 9 hadi 16.IMG_0164Maandamano ya vikundi mbalimbali kutoka katika Mkoa wa Kilimanjaro wakipita mbale ya mgeni rasmi Mama Salma Kikwete wakati wa sherehe ya uzinduzi wa chanjo kwenye uwanja wa Mandela huko Pasua mjini Moshi tarehe 28.4.2014.IMG_0168Maandamano ya vikundi mbalimbali kutoka katika Mkoa wa Kilimanjaro wakipita mbale ya mgeni rasmi Mama Salma Kikwete wakati wa sherehe ya uzinduzi wa chanjo kwenye uwanja wa Mandela huko Pasua mjini Moshi tarehe 28.4.2014.IMG_0185  Mamia ya watu waliohudhuria sharehe za uzinduzi wa chanjo ya kuzuia maambukizi ya saratani ya shingo ya kizazi kwa wasichana wakifuatilia kwa makini hotuba ya Mgeni rasmi, Mama Salma Kikwete katika sherehe hiyo.IMG_0228  Mamia ya watu waliohudhuria sharehe za uzinduzi wa chanjo ya kuzuia maambukizi ya saratani ya shingo ya kizazi kwa wasichana wakifuatilia kwa makini hotuba ya Mgeni rasmi, Mama Salma Kikwete katika sherehe hiyo.IMG_0236Mke wa Rais Mama Salma Kikwete akiwahutubia mamia ya wananchi na wanafunzi waliohudhuria sherehe za uzinduzi rasmi wa chanjo ya kuzuia saratani ya shingo ya kizazi kwa wasichana wenye umri wa miaka 9 hadi 16 huko Pasua, Moshi tarehe 28.4.2014.IMG_0303Mke wa Rais Mama Salma Kikwete akikata utepe kuashiria uzinduzi rasmi wa chanjo ya kuzuia maambukizi ya saratani ya shingo ya kizazi kwa wasichana kwenye sherehe iliyofanyika huko Pasua, Moshi Mjini tarehe 28.4.2014. Wengine katika picha (kushoto kwenda kulia) ni Ndugu Leonidas Gama, Mkuu wa Mkoa wa Kilimanjaro, Dkt. Rufaro Chatora, Mwakilishi wa Shirika la Afya Duniani hapa nchini, Dkt Kebwe Stephen Kebwe, Naibu Waziri wa Afya na Ustawi wa Jamii, Dkt. Neema Rusibamayila, Mkurugenzi wa Kinga kutoka Wizara ya Afya, Mama Salma na wa Kwanza kulia ni Mwakilishin wa Shirika la Kuhudumia watoto (UNICEF) hapa nchini  Dkt. Sudha Sharma.IMG_0332Mke wa Rais Mama Salma Kikwete akimwangalia muuguzi akitoa chanjo ya kuzuia saratani ya shingo ya kizazi kwa msichana Salma Abillah, 12, anayesoma darasa la 4 Shule ya Msingi Azimio huko Moshi mara baada ya Mama Salma kuzindua rasmi tarehe 28.4.2014.IMG_0350Mke wa Rais Mama Salma Kikwete akiandika taarifa za mtoto Salma Abillah mara baada ya kupata chanjo ya kuzuia saratani ya shingo ya kizazi na baadaye kumkabidhi kadi yake ambayo anatakiwa kurudi tarehe 28.10.2014 kwa ajili ya kupata chanjo ya pili.IMG_0373Mke wa Rais Mama Salma Kikwete anaonekana akitoa chanjo ya matone kuzuia ugonjwa wa polio kwa mtoto Ahmad, miezi 10, aliyefika kwenye sherehe ya uzinduzi wa chanjo ya kuzuia maambukizi ya saratani ya shingo ya kizazi kwa wasichana huko Pasua, Moshi tarehe 28.4.2014.
 PICHA NA JOHN  LUKUWI.

Serikali imetumia zaidi ya Shilingi Bilioni 111 kununua mazao kwa wakulima katika kipindi cha mwaka 2013/2014 ikiwa ni malipo kwa wakulima baada ya kuiuzia nafaka Serikali.

Afisa Mtendaji Mkuu wa Wakala wa Taifa wa Hifadhi ya Chakula Bw. Charles akiongea na waandishi wa Habari( Hawapo Pichani) kuhusu mafanikio yaliyopatikana na wakala hao ikiwamo kutumia Zaidi ya Bilioni 111 kununua mazao kwa wakulima katika kipindi cha Mwaka 2013/2014. wakati wa Mkutano uliofanyika katika ukumbi wa Idara ya Habari (MAELEZO) Jijini Dar es Salaam. Kulia ni Mkurugenzi Mipango na Uendeshaji wa wakala huo Bi. Anna Mapunda.
Baadhi ya waandishi wa Habari waliohudhuria Mkutano huo wakimsikiliza Afisa Mtendaji Mkuu wa Wakala wa Taifa wa Hifadhi ya Chakula Bw. Charles wakati wa Mkutano uliofanyika katika ukumbi wa Idara ya Habari (MAELEZO) Jijini Dar es Salaam.
Picha na Georgina Misama
--
Na Frank Mvungi
SERIKALI imetumia zaidi ya Shilingi Bilioni 111 kununua mazao kwa wakulima katika kipindi cha mwaka 2013/2014 ikiwa ni malipo  kwa wakulima  baada ya kuiuzia  nafaka Serikali.

Hayo yamesemwa na Afisa Mtendaji Mkuu wa Wakala wa Taifa wa Hifadhi ya Chakula (NFRA) Charles Walwa wakati wa mkutano na Waandishi wa Habari jana jijini Dar es salaam wakati alipokuwa akieleza mafanikio yaliyofikiwa na  wakala huo.
Walwa alisema kuwa wakala huo umeweza kuongeza kiasi cha nafaka zilizonunuliwa kutoka kwa wakulima kutoka  tani 61,587.784 mwaka 2008/2009 hadi tani 219,377.282 mwaka 2013/2014 ikiwa ni matokeo ya kuboreshwa kwa mifumo ya utendaji wa wakala huo.

“Hadi kufikia Desemba 31 mwaka 2013 wakala ulinunua tani 219,377.282 za nafaka sawa na asilimia 110 ambapo tani 218,878.600 ni mahindi na tani 498.682 ni mtama” alisema Walwa.

Aliongeza kuwa wakala umeingia makubaliano ya mashirikiano ( Memorandum  of Understanding(MOU)  na Shirika la Mpango wa Chakula Duniani (WFP) ili kuwahakikiishia wakulima soko la uhakika.

Katika kutekeleza makubaliano  na WFP  Walwa alisema kuwa wakala umeuza tani 80,000 mwaka 2011/2012 ambapo kwa sasa wakala unaendelea kutekeleza mkataba mwingine wa kuuza tani 23,000 kwa mwaka 2013/2014.

Katika hatua nyingineWalwa alisema kutokana na mfumo mzuri wa manunuzi ya nafaka kutoka kwa wananchi,  ajira za muda kwa wananchi takribani 3000 zizizalishwa na makundi mbalimbali ya wananchi wakati wa kukusanya nafaka tatika maeneo mbalimbali hapa nchini.

Wakala wa Taifa wa Hifadhi ya Chakula umepanga kuongeza uwezo wa kuhifadhi nafaka kutoka tani 241,000 za Sasa hadi tani  laki 400,000 ifikapo mwaka 2016 na Tani 700,000 ifikapo mwaka 2024

Rais Jakaya Kikwete katika Ikulu ya Dar es Salaam amekabidhi vitabu 2,181 kwa Jeshi la Wananchi wa Tanzania (JWTZ) kwa ajili ya vyuo vya Jeshi ili kuongeza taaluma.

Rais Jakaya Mrisho Kikwete  katika Ikulu ya Dar es Salaam amekabidhi vitabu 2,181 kwa Jeshi la Wananchi wa Tanzania (JWTZ) kwa ajili ya vyuo vya Jeshi ili kuongeza taaluma.

Rais amekabidhi vitabu hivyo kwa Mkuu wa Majeshi Jenerali Davis Mwamunyange na kuahidi kuendelea kutafuta vitabu zaidi kwa ajili ya kuboresha Maktaba ya Jeshi iliyopo katika Chuo Cha Kijeshi kilichopo Monduli, Mkoani Arusha.

Library hiyo ilianzishwa na Mheshimiwa Rais wakati alipokuwa mkufunzi katika chuo hicho miaka iliyopita.

"Lazima mtenge bajeti kwa ajili ya vitabu lakini na mimi nitaendelea kutafuta vitabu niwaletee ili kuijengea uwezo Library yetu ya Monduli”.

Akipokea vitabu hivyo kwa niaba ya Jeshi, Jenerali Mwamunyange amemshukuru Rais kwa juhudi zake za kuboresha Jeshi la Wananchi Tanzania kwa ujumla na kulifanya kuwa la kisasa zaidi. 

“Juhudi zako za kuliendeleza Jeshi letu imetuongezea uwezo na kujiamini zaidi. Bila juhudi zako tusingefika hapa tulipo na tunajivunia sana mafanikio haya”
 amesema Jenerali Mwamunyange .
Imetolewa na;
Premi Kibanga,
Mwandishi wa Habari wa Rais Msaidizi,
Ikulu – Dar es Salaam.
 28 Aprili,2014

Wastaafu Watakiwa Kuhakiki Taarifa Zao Za Fao ya Uzeeni

Meneja Uhusiano na Masoko kutoka Mfuko wa Pensheni wa PPF Bi. Lulu Mengele akiongea na waandishi wa Habari ( Hawapo Pichani) kuhusu wastaafu kwenda kuhakiki taarifa za mafao katika Ofisi za Mfuko huo, wakati wa Mkutano uliofanyika katika ukumbi wa Idara ya Habari (MAELEZO)  Jijini Dar es Salaam. Kulia ni Afisa Habari wa Idara ya Habari (MAELEZO) Bw. Frank Mvungi
Baadhi ya waandishi wa Habari waliohudhuria Mkutano huo wakimsikiliza Meneja Uhusiano na Masoko kutoka Mfuko wa Pensheni wa PPF Bi. Lulu Mengele wakati wa Mkutano uliofanyika katika ukumbi wa Idara ya Habari (MAELEZO) Jijini Dar es Salaam. Picha na Georgina Misama

MAKAMU WA RAIS DK GAHRIB BILAL MGENI RASMI MAADHIMISHO YA SIKU YA USALAMA NA AFYA DUNIANI

  Watumishi wa taasisi mbalimbali wakiwa kwenye maandamano ya maadhimisho ya siku ya Usalama na Afya Duniani yaliyoadhimishwa jana April 28-2014 kwenye viwanja vya mnazi mmoja jijini Dar es salaam.
 Watumishi wa taasisi mbalimbali wakiwa kwenye maandamano ya maadhimisho ya siku ya Usalama na Afya Duniani yaliyoadhimishwa janaApril 28-2014 kwenye viwanja vya mnazi mmoja jijini Dar es salaam.
 Watumishi wa taasisi mbalimbali wakiwa kwenye maandamano ya maadhimisho ya siku ya Usalama na Afya Duniani yaliyoadhimishwa jana April 28-2014 kwenye viwanja vya mnazi mmoja jijini Dar es salaam.
 Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akisalimiana na viongozi mbalimbali alipowasili kwenye viwanja vya mnazi mmoja jijini Dar es salaam jana April 28-2014, kwa ajili ya kuhutubia wananchi kwenye maadhimisho ya siku ya usalama na Afya Duniani.
  Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akipokea maandamano kwenye maaadhimisho ya siku ya Usalama na Afya yaliyoadhimishwa jana April 28-2014  katika viwanja vya mnazi mmoja jijini Dar es salaam.
 Afisa mkuu mwandamizi wa mazingira katika mamlaka ya Bandari Thobias Sonda akimpa maelezo Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Mohammed Gharib Bilal, juu ya utumiaji wa vifaa vya kupimia hewa, wakati alipotembelea Banda la maabara ya mkemia mkuu wa Serikali kwenye Maonesho ya maadhimisho ya siku ya Usalama na Afya  Duniani yaliyoadhimishwa jana April 28-2014, Viwanja vya Mnazi mmoja jijini Dar es salaam. 
 Mtaalam wa uchunguzi wa vyakula katika maabara ya mkemia mkuu wa Serikali Edith Wilbald akimpa maelezo Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Mohammed Gharib Bilal, wakati alipotembelea Banda la maabara ya uchunguzi wa vyakula kwenye Maonesho ya maadhimisho ya siku ya Usalama na Afya  Duniani.
  Mtaalam wa uchimbaji wa madini katika mgodi wa Noth Mara Gold Mine Paul Kagodi akimuonesha Makamu wa Rais vifaa vinavyotumika katika kazi ya uchimbaji wa madini wakati alipotembelea mabanda ya Maonesho kwenye maadhimisho ya siku ya Usalama na Afya  Duniani yaliyoadhimishwa jana.

  Katibu Mkuu wa Shirikisho la Wafanyakazi Nicolas Mgaya akizungumza kwenye maadhimisho ya siku ya Usalama na Afya Mahali pa kazi Duniani  yaliyoadhimishwa jana April 28-2014  katika viwanja vya mnazi mmoja jijini Dar es salaam.
  Makamu wa Rais, Dkt. Bilal, akihutubia kwenye hafla hiyo.
  Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akimkabizi zawadi maalum Naibu Waziri wa Kazi na Ajira Mhe. Makongoro Mahanga wakati wa  maaadhimisho ya siku ya Usalama na Afya Mahali pa kazi Duniani yaliyoadhimishwa jana April 28-2014  katika viwanja vya mnazi mmoja jijini Dar es salaam.
  Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akimkabizi zawadi K. Lwakatare mkuu wa usalama na mazingira Vodacom kwenye maadhimisho ya siku ya Usalama na Afya yaliyoadhimishwa jana April 28-2014  katika viwanja vya mnazi mmoja jijini Dar es salaam.
  Picha ya pamoja...
  Wanamuziki wa bendi ya 'OUT Jaz Band' wakitumbuiza kwenye maadhimisho ya siku ya Usalama na Afya Mahali pa kazi Duniani  yaliyoadhimishwa jana.Picha na Ofisi ya Makamu wa Rais

VETA YAENDESHA SEMINA KWA WABUNGE WA KAMATI YA KUDUMU YA BUNGE YA HUDUMA ZA JAMII JUU YA MRADI WA KUONGEZA SIFA ZA KUAJILIWA - EEVT JIJINI DAR

Mkurugenzi Mkuu wa VETA, Mh Mhandisi Zebadiah Moshi akiongea wakati wa semina iliyoandaliwa na VETA kwaajili ya Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Huduma za Jamii 
Mh Jenista Mhagama (Kushoto) akiongea na baadhi ya wabunge kutoka Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Huduma za Jamii na baadhi ya wafanyakazi wa VETA kutoka Makao Makuu na VETA Kanda ya Kusini wakati wa semina iliyoandaliwa na VETA   Kwaajili ya wabunge wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Huduma za Jamii juu ya mradi wa Kuongeza sifa za kuajiliwa - EEVT iliyofanyika katika Ukumbi wa Benki wa Kuu ya Tanzania, Jijini Dar Es Salaam. Katikati ni Mwenyekiti wa Kamati hiyo Mh Magreth Sitta na Kulia ni Steven Ngonyani.
Mwenyekiti wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Huduma za Jamii, Mh Magreth Sitta (Katikati) akiongea wakati wa semina iliyoandaliwa na VETA kwaajili ya Kamati hiyo iliyofanyika katika Ukumbi wa Benki kuu ya Tanzania Jijini Dar Es Salaam.
 Mkurugenzi Mkuu wa VETA Tanzania, Mh Mhandisi Zebadiah Moshi(kulia) akifungua semina iliyoandaliwa na VETA kwaajili ya Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Huduma za Kijamii katika Ukumbi wa Benki Kuu ya Tanzania.
Mkurugenzi wa Soko la Ajira, Mipango na Maendeleo Kutoka VETA, Bw Enock Kibendela akitoa mada juu ya mchango mkubwa unaotolewa na VETA Katika kukuza sekta ya ajira kwa vijana wanaopata mafunzo ya ufundi stadi wakati wa semina iliyoandaliwa na VETA kwa wabunge wa kamati ya Kudumu ya Bunge ya Huduma za Jamii katika ukumbi wa Benki Kuu ya Tanzania.
Baadhi ya wabunge wa kamati ya kudumu ya Bunge ya Huduma za Jamii pamoja na wafanyakazi wa VETA waliohudhuria semina iliyoandaliwa na VETA Kwaajili ya wabunge wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Huduma za Jamii juu ya mradi wa Kuongeza sifa za kuajiliwa - EEVT.

WIZARA YA ARDHI YAPONGEZWA KUTENGA FEDHA KUKAMILISHA MRADI WA MAKTABA

Kamati ya Bunge ya Ardhi, Maliasili na Utalii imeipongeza Wizara ya Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi kwa kutenga fedha kiasi cha Shiling...