Friday, January 11, 2008

Sikia kituko cha kondomu

TBS yakataa kondomu fupi

Na Tausi Mbowe na Sophia Mlenda

SHIRIKA la Viwango Tanzania (TBS), limelazimia kurudisha kondomu zilizoingizwa nchini baada ya kugundulika kuwa ni fupi ambazo haziliganini na urefu unaotakiwa.

Akizungumza katika ziara ya Waziri Mkuu, Edward Lowassa, Mtaalamu Mwandamizi wa Maabara wa TBS, Mary Mlembe alisema kuwa kondomu hizo ziliingizwa nchini kutoka nchini Korea.

Mlembe ambaye alikuwa akitoa maelezo kwa Waziri Mkuu juu ya ubora wa kondomu na jinsi ya kuzifanyia uchunguzi alisema baada ya kufanyiwa uchunguzi kondomu hizo ziligundulika kuwa zilikuwa hazikidhi viwango vya kimataifa vinavyokubalika kwa kuwa zilikuwa fupi.

"Kuna wakati TBS tulipokea Kondomu kutoka nchini Korea lakini baada ya kuzifanyia uchunguzi tuligundua kuwa hazikidhi viwango vya kimataifa kwa kuwa zilikuwa fupi ulikinganisha na urefu unaohitajika," alisema Mlembe.

Alisema katika kupima ubora wa kondomu hizo TBS hutumia viwango vilivyowekwa kimataifa ambavyo vinakubalika na nchi mbalimbali.

Alisema katika ukaguzi huo kondomu hizo hupimwa ili kujua uwezo wa kondomu hizo katika ujazo na uzito, kupima matundu kama inaruhusu hewa na kupima kama imefungwa vizuri ili isiruhusu kupitisha hewa pamoja na kujua upana na unene.

Alisema kwa sasa viwango vinavyokubalika kimataifa ni urefu usiopungua nchi 160 na kuendelea na upana wa nchi 53 wakati unene unatakiwa kuwa sentimita 0.07.

Alisema baada ya kukagua kondomu hizo Shirika hilo lilijiridhisha kuwa viwango vyake havikufikia ubora kwa kuwa zilikuwa fupi kuliko inavyohitajika.

Alisema sheria ya shirika hilo inatamka wazi kuwa bidhaa isiokidhi ubora wa viwango vilivyowekwa kitaifa au kimataifa bidhaa hizo hulazimika kurejeshwa sehemu ilipotoka hivyo TBS ililazimka kurudisha bidhaa hizo kwa kuwa si salama kwa mtumiaji.
Hata hivyo, Mlembe alisema mara nyingi shirika lake linapata bidhaa za kondomu ambazo hazikidhi viwango vilivyowekwa na shirika hilo hivyo kulazimika kurejeshwa sehemu zilizotoka

No comments:

WIZARA YA ARDHI YAPONGEZWA KUTENGA FEDHA KUKAMILISHA MRADI WA MAKTABA

Kamati ya Bunge ya Ardhi, Maliasili na Utalii imeipongeza Wizara ya Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi kwa kutenga fedha kiasi cha Shiling...