Tuesday, January 22, 2008

Watuhumiwa wa kumshambulia Kubenea hawa hapa





WATU watano wamefikishwa katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu, jijini Dar es Salaam kujibu tuhuma za kuvamia ofisi za gazeti la MwanaHalisi na kummwagia kemilikali inayodhaniwa kuwa tindikali Mhariri Mtendaji wa gazeti hilo Saed Kubenea na kumjeruhi kwa sime Mhariri wake wa habari, Ndimara Tegambwage.

Mwendesha Mashtaka Mkuu wa Polisi, Charles Kenyela aliwataja washtakiwa hao mbele ya Hakimu Mkazi wa Mahakama hiyo Addy Lyamuya kuwa ni Alex Mwandemele (28) maarufu kwa jina la Chusa wa Kigogo na Hashim Mndoe (32) maarufu kwa jina la Madilu wa Tegeta.

Wengine ni Augustino Joseph (30) maarufu kwa jina la Cheusi wa Mwananyamala, Hamis Ramadhani (25) wa Mwananyamala na mkazi wa Kinondoni Alfred Moshi (64), maarufu kwa jina Chambya.

Kenyela alidai mahakamani hapo kuwa washtakiwa hao kwa pamoja wanakabiliwa na makosa ya kula njama ya kujeruhi, kummwagia tindikali Kubenea na kumjeruhi Ndimara Tegambwage.

1 comment:

Anonymous said...

I am really impressed with your writing skills and also
with the layout on your weblog. Is this a paid theme or did you modify it
yourself? Either way keep up the excellent quality writing,
it is rare to see a great blog like this one today.
http://www.iwapu.com/index.php?do=/blog/9475/the-best-way-to-decide-the-right-time-period-of-tuition-insurance-policy/
http://dreamcardatematch.com/groups/determine-begin-using-home-singapore-tuition-onto-your-teenager/

my website - american samoa tsunami

SAMIA AZINDUA MKUTANO WA KIMATAIFA WA WFNS, ATEMBELEA MAONESHO YA SEKTA YA AFYA

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan, akitembelea mabanda ya maonesho ya wadau wa Sekta ya Afya kabla ya k...