Saturday, January 05, 2008

bongo kama kenya

Picha ya Edwin Mujwahuzi

JAMAA wa CHADEMA leo walitaka kufanya mambo fulani hivi kama kule Kenya wakaazimia kuandamana kuwatetea ndugu zao wa Kenya kina Odinga jeshi la Polisi jijini Dar es Salaam jana likatawanya maandamano yaliyokuwa yamepangwa na vyama vinne vya upinzani yaliyolenga kupinga ushindi wa Rais wa Kenya, Mwai Kibaki na kumtaka kuachia ngazi ili kurejesha amani nchini humo.

Maandamano hayo yalikuwa yanaratibiwa na Makamu Mwenyekiti wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), Chacha Wangwe na yalipangwa kuanza saa mbili asubuhi katika eneo la Urafiki, Manzese jijini Dar es Salaam na kumalizikia katika ofisi za Ubalozi wa Kenya nchini.

No comments:

WIZARA YA ARDHI YAPONGEZWA KUTENGA FEDHA KUKAMILISHA MRADI WA MAKTABA

Kamati ya Bunge ya Ardhi, Maliasili na Utalii imeipongeza Wizara ya Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi kwa kutenga fedha kiasi cha Shiling...