Tuesday, January 15, 2008

Mabucha ya nyama kupigwa marufuku Tanzania

Na Muhibu Said wa Mwananchi

SERIKALI inapanga kupiga marufuku uuzaji nyama kwenye mabucha na badala yake biashara hiyo itakuwa ikifanywa na maduka makubwa (supermarkets) na maeneo maalum yatakayotengwa nchini.

Mpango huo mpya ambao serikali imedhamiria kuutekeleza kwa dhati wakati wowote katika siku za usoni, ulitangazwa na Waziri wa Maendeleo ya Mifugo, Anthony Diallo, alipozungumza na waandishi wa habari ofisini kwake, jijini Dar es Salaam jana.

Waziri Diallo alisema mpango huo umelenga kukidhi mahitaji ya afya za walaji wa nyama na soko la nje la bidhaa hiyo na kwa kuzingatia hilo, wizara yake inafanya mazungumzo na halmashauri ili waweze kuanza kuutekeleza.

Alisema utayarishaji wa nyama katika mabucha unaofanywa kwa ajili ya kuwauzia walaji hivi sasa, umekuwa ukitishia afya zao kutokana na wauzaji kutumia nyenzo zilizotumika kwa muda mrefu, kama vile magogo ya kucharangia nyama, ambayo ubora wake haukidhi mahitaji ya afya.GAZETI LA MWANANCHI ili mpate taarifa zaidi

No comments:

WIZARA YA ARDHI YAPONGEZWA KUTENGA FEDHA KUKAMILISHA MRADI WA MAKTABA

Kamati ya Bunge ya Ardhi, Maliasili na Utalii imeipongeza Wizara ya Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi kwa kutenga fedha kiasi cha Shiling...