Friday, January 04, 2008

Barua ya Wazi ya Profesa Shivji kwa JK, Museveni

Barua ya wazi kwa Marais Kikwete, Kagame na Kaguta juu ya hali ya Wakenya

Ninashindwa kuwasalimia kwa kheri za mwaka mpya. Katika eneo letu hili la Afrika, hakuna heri, kuna shari tu. Waafrika wenzetu huko Kenya wanakufa bila sababu. Sababu ni moja tu – uchu wa madaraka. Inanishangaza sana kwamba nyie kama viongozi wa nchi za Afrika zinazoshirikiana katika Jumuiya ya Afrika Mashariki yenye lengo la kujenga msingi wa Shirikisho la Afrika, mko kimya. Huu sio wakati wa kucheza mchezo wa kidiplomasia.

Hatutaki, hatutaki kabisa kuona tena jangwa la maauaji ya halaiki yatokee barani Afrika. Tumechoka kuona wanaadamu, Waafrika wenzetu, wakiuawa kama wanyama mitaani na hao wanaojiita eti vyombo vya usalama. Usalama wa nani kama sio wa wananchi?

Jukumu la awali kabisa la vyombo hivyo ni kulinda usalama wa raia; kutuliza ghasia sio kuchochea ghasia au chuki. Wakiwakuta waandamaji bila silaha wawalinde, wawashauri kufanya maandamano yao kwa amani, wawapatie nafasi ya kuonyesha madukuduku yao kuhusu uchaguzi. Bonyeza
hapa upate kusoma uchambuzi huu zaidi.

No comments:

WIZARA YA ARDHI YAPONGEZWA KUTENGA FEDHA KUKAMILISHA MRADI WA MAKTABA

Kamati ya Bunge ya Ardhi, Maliasili na Utalii imeipongeza Wizara ya Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi kwa kutenga fedha kiasi cha Shiling...