BALOZI WA KUWAIT NCHINI TANZANIA AZUNGUMZA NA WAZIRI WA AFYA KUHUSU MRADI WA MATENGENEZO YA HOSPITALI KUU YA MNAZIMMOJA.
Waziri wa Afya Mahamoud Thabit Kombo akizungumza na Balozi wa Kuwait nchini Tanzaania Jasem Al Najim alipomtembelea Ofisini kwake kumuelezea juu ya Mradi wa kuifanyia matengenezo makubwa Hospitali Kuu ya Mnazimmoja, Mjini Zanzibar.
Waziri wa Afya Mahamoud Thabit Kombo akiwa na mgeni wake Balozi wa Kuwait nchini Tanzania akimtembelea Hospitali Kuu ya Mnazimmoja ambayo itafanyiwa matengenezo makubwa na Serikali ya nchi hiyo.
Waziri wa Afya Mahmoud Thabit Kombo na Balozi wa Kuwait nchini Tanzania wakitembelea wagonjwa waliolazwa katika wodi ya wanaume waliopata ajali katika Hospitali Kuu ya Mnazimmoja.
Balozi wa Kuwait Jasem Al-Njim akiangali chumba cha kuhifadhia maiti (mortuary) ya Hospitali Kuu ya Mnazimmoja ambapo alisema sehemu hiyo itakuwa ya kwanza kufanyiwa matengenezo makubwa.Balozi wa Kuwait Jasem Al-Njim akiangali chumba cha kuhifadhia maiti (mortuary) ya Hospitali Kuu ya Mnazimmoja ambapo alisema sehemu hiyo itakuwa ya kwanza kufanyiwa matengenezo makubwa.
……………………………………………………………………………………………………….
NA RAMADHANI ALI-MAELEZO ZANZIBAR
Serikali ya Kuwait itayafanyia matengenezo makubwa majengo yote makongwe ya Hospitali Kuu ya Mnazimmoja, mradi utakaogharimu zaidi ya shilingi bilioni 84 za Tanzania.
Akizungumza na Waziri wa Afya Mahmoud Thabit Kombo Ofisini kwake Mnazimmoja, Balozi wa Kuwait nchini Tanzania Jasim Al-Najim alisema Serikali ya nchi yake tayari imekubali kutekeleza mradi huo haraka iwezekanavyo.
Alisema timu ya wataalamu kutoka Kuwait inatarajiwa kuwasili Zanzibar mwezi Ogasti kwa ajili ya kufanya uchunguzi yakinifu na kazi za matengenezo ya Hospitali zitaanza mara tu baada ya wataalamu hao kumaliza kazi hiyo.
Aliongeza kuwa kufanikiwa kwa mradi huo mkubwa utafungua milango kwa Serikali ya Kuwait kupitia Mashirika ya misaada ya nchi hiyo kusaidia miradi mengine midogo midogo na vifaa kwa ajili ya maendeleo ya sekta ya Afya na sekta nyengine za kiuchumi na kijamii.
Balozi Al-Nagim alisema hatua hiyo ni kuonyesha umoja, ushirikiano na mapenzi ya dhati yaliopo kati ya Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar na Serikali ya Kuwait.
Waziri wa Afya Mahmoud Thabit Kombo aliishukuru Serikali ya Kuwait kwa kukubali kutekeleza mradi huo mkubwa ambao utawasaidia wananchi wote wa Zanzibar.
Aidha alizishukuru Wizara za Fedha za Serikali ya Muungano wa Tanzania na Serikali ya Mpinduzi ya Zanzibar, ambazo zilikubali kutekelezwa kwa mradi huo ndani ya Wizara ya Afya.
Balozi Al-Najim alipata nafasi ya kutembelea baadhi ya wodi za kulaza wagonjwa na sehemu ya kuhifadhia maiti ya Hospitali Kuu ya Mnazimmoja, ambapo kutokana na kuguswa na sehemu hiyo, alisema itakuwa ya kwanza kufanyiwa matengenezo mradi huo utakapoanza.

Comments