Mwenyekiti wa Gidani Group na Makamu wa Rais wa Shirikisho la Michezo ya kubahatisha katika kanda ya Afrika ya Kusini Profesa Bongani Aug Khumalo akielezea jinsi michezo ya Bahati Nasibu itakavyoendeshwa kwa wananchi waliofika kwenye Banda la Maonyesho ya Kimataifa ya Biashara ambapo kampuni hiyo ilishiriki
Mkurugenzi wa Bodi inayosimamia michezo ya Kubahatisha nchini,Bw, Abbas Tarimba akiwa na Mwenyekiti wa Gidani Group ,Profesa Bongani Aug Khumalo
……………………………………………………………………………………….
*Mshindi kujinyakulia kitita cha shilingi milioni 100
Mchezo mkubwa wa kubahatisha nchini wa Bahati Nasibu ya Taifa utaanza kuchezwa nchini mwezi huu na tiketi za kushiriki zitaanza kuuzwa katika mikoa yote kuanzia Mei 21 mwezi huu ambapo droo ya kwanza itafanyika Mei 28 ambapo mshindi wa zawadi kubwa atakuwa milionea kwa kijishindia kitita cha shilingi milioni 100.
Mchezo huu kwa sasa utaendeshwa na kampuni ya kimataifa ya michezo ya Bahati Nasibu ya Gidani International ambayo kupitia kampuni yake tanzu ya Murhandizwa Limited mwaka jana ilipata leseni ya kuendesha michezo ya bahati nasibu ya Taifa nchini na kwa muda wote imekuwa ikijenga mazingira ya kuendesha michezo hii kisasa kutokana na uzoefu wake mkubwa wa kuiendesha katika nchi mbalimbali.
Bahati Nasibu ya Taifa itachezesha michezo mikubwa itakayowezesha washiriki kushinda zawadi kubwa katika mwaka wake wa kwanza wa kuendesha shughuli zake hapa nchini sambamba na kuweka rekodi barani Afrika na sehemu nyinginezo duniani.
“Katika kusherehekea kuanza kwa bahati nasibu hii hapa nchini katika michezo ya 6 ya mwanzoni itazalisha mamilionea kwa kuwa washindi wa droo kubwa watanyakua zaidi ya milioni 1000.Tunategemea maisha ya watu wengi yatabadilika kuwa bora kupitia bahati nasibu huu pia usambazaji wa tiketi utafanyika kwa utaalamu mkubwa”.Alisema Profesa Bongani Aug Khumalo, Mwenyekiti wa Gidani Group na Makamu wa Rais wa Shirikisho la Michezo ya kubahatisha katika kanda ya Afrika ya Kusini.
Tiketi za kushiriki bahati nasibu hii itauzwa shilingi 500 kila moja na zitapatikana nchi nzima kupitia mtandao wa mawakala wa kampuni pia zitauzwa kwa njia ya mtandao.Maelezo zaidi ya kushiriki yatatolewa kupitia vyombo vya habari wakati wa kuuza tiketi ukifika.
Kwa maelezo zaidi tembelea tovuti ya www.nationallottery .co.tz kuanzia Mei 9,pia taarifa na matangazo juu ya mchezo huu yatapatikana kwenye vyombo vya habari.
No comments:
Post a Comment