Monday, May 09, 2016

SUMATRA YATANGAZA NAULI ZA USAFIRI WA MABASI YAENDAYO HARAKA

S1
Meneja Mawasiliano wa Mamlaka ya Udhibiti Usafiri wa Majini na Nchi Kavu (SUMATRA) Bw. David Mziray akitoa ufafanuzi kwa waandishi wa habari (hawapo pichani) wakati wa mkutano wa wadau wa usafiri wakiwamo SUMATRA, UDA, DART na Jeshi la Polisi.
S2Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Udhibiti Usafiri wa Majini na Nchi Kavu (SUMATRA) Bw. Giliard Ngewe akiongea na waandishi wa Habari (hawapo pichani) kuhusu nauli zitakazotumika katika mradi wa mabasi yaendayo haraka unaotarajiwa kuanza rasmi Mei 10, 2016. Kushoto ni Mkurugenzi wa Udhibiti Uchumi kutoka SUMATRA Bw. Nahson Sigala.
S3Mkurugenzi wa Udhibiti Uchumi wa Mamlaka ya Udhibiti Usafiri wa Majini na Nchi Kavu (SUMATRA) Bw. Nahson Sigala akiwaeleza waandishi wa habari kuhusu viwango vipya vya nauli baada ya SUMATRA kufanya tathmini ya viwango vya nauli iliyopendekezwa awali na Kampuni ya Usafirishaji ya UDA-RT na kubaini kuwa gharama zilizopendekezwa ni kubwa mno. Kulia ni Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Udhibiti Usafiri wa Majini na Nchi Kavu (SUMATRA) Bw. Giliard Ngewe.
S4Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Udhibiti Usafiri wa Majini na Nchi Kavu (SUMATRA) Bw. Giliard Ngewe (Kulia) na Kaimu Mtendaji Mkuu DART Bw. Ronald Lwakatare wakimkabidhi leseni ya usafirishaji Mkurugenzi Mtendaji wa Kampuni ya Usafirishaji ya UDA-RT Bw. David Mgwassa (Katikati).
S5Mkurugenzi Mtendaji wa Kampuni ya Usafirishaji ya UDA-RT Bw. David Mgwassa (Kushoto) akimshukuru Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Udhibiti Usafiri wa Majini na Nchi Kavu (SUMATRA) Bw. Giliard Ngewe baada ya kupokea leseni ya usafirishaji kutoka SUMATRA.
PICHA NA FATMA SALUM-MAELEZO

No comments:

WIZARA YA ARDHI YAPONGEZWA KUTENGA FEDHA KUKAMILISHA MRADI WA MAKTABA

Kamati ya Bunge ya Ardhi, Maliasili na Utalii imeipongeza Wizara ya Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi kwa kutenga fedha kiasi cha Shiling...