Sunday, May 08, 2016

RAIS DKT. MAGUFULI ATUNUKU KAMISHENI MAAFISA 586 KATIKA CHUO CHA MAAFISA WA JESHI MONDULI

MON1
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Amiri Jeshi mkuu Dkt. John Pombe Magufuli akikagua gwaride kabla ya kutunuku Kamisheni kwa Maafisa Wapya 586 wa jeshi la Wananchi wa Tanzania kundi la 58/15 katika chuo cha kijeshi cha Monduli TMA mkoani Arusha.
MON2Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Amiri Jeshi mkuu Dkt. John Pombe Magufuli akikagua gwaride kabla ya kutunuku Kamisheni kwa Maafisa Wapya 586 wa jeshi la Wananchi wa Tanzania kundi la 58/15 katika chuo cha kijeshi cha Monduli TMA mkoani Arusha.
MON3Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Amiri Jeshi mkuu Dkt. John Pombe Magufuli akitunuku kamisheni kwa maafisa wapya 586 wa jeshi la Wananchi wa Tanzania kundi la 58/15 katika chuo cha Mafunzo ya kijeshi cha Monduli TMA mkoani Arusha
MON4Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Amiri Jeshi mkuu Dkt. John Pombe Magufuli akimpongeza Afisa Mpya wa cheo cha Luteni Usu, Nasra Rashid ambaye alifanya vizuri zaidi kuliko Maafisa Wanafunzi wanawake katika chuo cha kijeshi cha Monduli TMA mkoani Arusha.
MON5Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Amiri Jeshi mkuu Dkt. John Pombe Magufuli akisalimiana na Mkuu wa Majeshi ya Ulinzi ya wananchi General Davis Mwamunyange mara baada ya kuwasili kwenye chuo cha Mafunzo Kijeshi cha Monduli TMA mkoani Arusha.
MON6Maafisa Wanafunzi wakipita kwa mwendo wa haraka  mbele ya Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Amiri Jeshi mkuu Dkt. John Pombe Magufuli kabla ya kutuniwa Kamisheni
MON7Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Amiri Jeshi mkuu Dkt. John Pombe Magufuli akizungumza jambo na Mkuu wa Chuo cha Mafunzo ya Kijeshi cha Monduli TMA Meja Jenerali Paul Peter Massao kabla ya kutunuku Kamisheni kwa Maafisa Wapya 586 katika chuo hicho cha Monduli.
MON8Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Amiri Jeshi mkuu Dkt. John Pombe Magufuli akiwa katika picha ya pamoja na baadhi ya Maafisa wapya aliowatunuku Kamisheni katika cha Mafunzo Kijeshi cha Monduli TMA mkoani Arusha. Wengine katika picha ni Mkuu wa Majeshi ya Ulinzi ya wananchi  Jeneral Davis Mwamunyange , Mkuu wa Chuo cha Mafunzo ya Kijeshi cha Monduli TMA Meja Jenerali Paul Peter Massao, Waziri wa Ulinzi Dkt. Hussein Mwinyi pamoja na Maafisa wa ngazi za juu katika Jeshi la Ulinzi.
MON9Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Amiri Jeshi mkuu Dkt. John Pombe Magufuli akiwasalimia wananchi  wa Ngarenaro waliomsimamisha wakati akitokea kwenye chuo cha Mafunzo ya Kijenshi cha Monduli mkoani Arusha.
MON10Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Amiri Jeshi mkuu Dkt. John Pombe Magufuli akitembea kikakamavu mara baada ya kutoka kukagua gwaride katika Chuo cha Mafunzo ya Kijeshi cha Monduli TMA mkoani Arusha.
MON11Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Amiri Jeshi mkuu Dkt. John Pombe Magufuli akisisitiza jambo wakati akizungumza na wanaanchi wa kona ya Mbauda mkoani Arusha.
MON12Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Amiri Jeshi mkuu Dkt. John Pombe Magufuli akifurahia jambo na Mkuu wa majeshi ya Ulinzi Jenerali Davis Mwamunyange katika Chuo cha Mafunzo ya Kijeshi cha Monduli mara baada ya kutazama picha za Majenerali wastaafu waliongoza Jeshi la Wananchi katika miaka ya nyuma.Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Amiri Jeshi mkuu Dkt. John Pombe Magufuli akifurahia jambo na Mkuu wa majeshi ya Ulinzi Jenerali Davis Mwamunyange katika Chuo cha Mafunzo ya Kijeshi cha Monduli mara baada ya kutazama picha za Majenerali wastaafu waliongoza Jeshi la Wananchi katika miaka ya nyuma.
MON13Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Amiri Jeshi mkuu Dkt. John Pombe Magufuli akizungumza na wakazi wa Kona ya Nairobi eneo la Arusha Tech mara baada ya kutoka kutunuku Kamisheni kwa maafisa Wapya katika Chuo cha Mafunzo ya Kijeshi  cha Monduli mkoani Arusha. PICHA NA IKULU
…………………………………………………………………………………………………..
Na Mahmoud Ahmad,Monduli
Amiri jeshi mkuu na Rais   wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dk.John Pombe Magufuli amewatunuku Kamisheni  wahitimu wapatoa 586 kutoka Chuo cha Kijeshi TMA kilichopo Monduli Mkoani Arusha.
Raisi dkta jpm ambaye hii ni mara ya pili kuwatunuku maofisa hao wakijeshi katika chuo hicho cha kijeshi aliweza kuwapa zawadi mbalimbali kwa wale waliofanya vizuri katika mafunzo yao.
Aidha Raisi Magufuli alifurahiswa na kitendo cha Askari wanawake wapatao 6 miongoni mwa wahitimu 586 waliopata fursa ya kutunukiwa vyeo na kuibua shangwe na nderemo kwa wageni waliohudhuria Kamisheni hiyo
“Leo (jana) nimewatunuku vyeo vya kuwa watumishi katika Jeshi la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kwa nafasi hiyo naomba Mungu awasaidie’’alisema Raisi wakati akiwatunuku
Kwa upande wake Mkuu wa Chuo hicho cha kijeshi TMA Meja Jenerali Paul Masau akitoa taarifa fupi juu ya mafunzo ya wahitimu hao mbele ya Rais Magufuli  kuwa wahitimu wote waliohitimu mafunzo hayo ni Raia wa Tanzania.
Aliongeza kuwa kati ya wahitimu hao  kuna marubani ,Madaktari,na wengi wao ni wahitimu wa kidato cha sita katika masomo ya Sayansi  ambao watakuja kuongeza ufanisi kwa utendaji kazi katika jeshi kwa siku za usoni ili jeshi hilo liende kisasa zaidi.
‘’Miongoni mwa wahitimu wapo madaktari 80, marubani  6 wa ndege,huku 500 ni vijana ambao wamehitimu kidato cha sita katika masomo ya Sayansi na kufaulu vizuri ambao watasaidia katika kulijenga zaidi jeshi letu kwa siku za usoni’’alisema Meja Jenerali Masau.

No comments:

WIZARA YA ARDHI YAPONGEZWA KUTENGA FEDHA KUKAMILISHA MRADI WA MAKTABA

Kamati ya Bunge ya Ardhi, Maliasili na Utalii imeipongeza Wizara ya Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi kwa kutenga fedha kiasi cha Shiling...