Naibu Katibu Mkuu wa UVCCM Zanzibar, Shaka Hamdu Shaka akiwahutubia mamia ya vijana katika moja ya mikutano ya umona huo kisiwani Zanzibar.
……………………………………………………………………………………………………..
Na Mwandishi Wetu, Zanzibar.
UMOJA wa vijana wa Chama cha Mapinduzi(UVCCM) Zanzibar umewataka vijana wa umoja huo katika Mkoa wa Kaskazini Unguja kuwakumbusha viongozi waliopo madarakani kwa sasa kutekeleza kwa haraka ahadi walizotoa wakati wa kuomba ridhaa ya kuingia madarakani katika Uchaguzi Mkuu wa Marudio uliofanyika mwaka huu.
Umesema vijana wana haki ya kutumia vikao halali vinavyokubalika katika utaratibu wa kiuongozi ndani ya UVCCM kuwakumbusha viongozi wa chama hicho kutekeleza kwa vitendo ahadi walizotoa kwa wananchi wa Zanzibar.
Akizungumza katika ziara ya UVCCM katika Mkoa huo, Kaimu Naibu Katibu Mkuu wa UVCCM Zanzibar, Abdulghafar Idrissa huko katika ofisi ya jimbo la Jimbo la Kitope iliyopo Kinduni Unguja.
Alifafanua kwamba CCM ni chama chenye viongozi makini wanaoahidi na wakatekeleza hivyo hakuna haja ya vijana kuendelea kulalamika badala yake wafuate utaratibu kuwakumbusha wahusika watekeleze majukumu yao kwa wananchi.
“ Vijana kumbukeni kuwa kwamba nyie ndiyo mliowaweka madarakani hao Marais, wabunge, wawakilishi na madiwani hivyo msiwaogope kuwakumbusha kwa kufuata taratibu wajibu wao wa kutekeleza ahadi zao kwenu na wakikataa basi rudini kwetu mtwambie na tutayafanyia kazi.”, alisema Idrissa.
Idrissa alisisitiza vijana hao kuendelea kuwa wamoja ili waweze kunufaika na fursa mbali mbali zilizopo katika chama na serikali iliyopo madakani.
Alisema umoja na mshikamano ndiyo njia pekee itakayowawezesha vijana kubuni fursa za maendeleo kwa lengo la kujikwamua katika wimbi la umasikini nchini.
No comments:
Post a Comment