Saturday, May 21, 2016

WATUMISHI WA UMMA 210 WAIDHINISHIWA MIKOPO YA NYUMBA YENYE THAMANI YA SHILINGI BILIONI 2.3

chaw2Na Tiganya Vincent-MAELEZO-Dodoma
Wizara ya Ardhi , Nyumba na Maendeleo ya Makazi imesema jumla ya Watumishi wa Serikali 210 wameidhinishiwa mikopo nyumba yenye thamani shilingi bilioni 2.3 baada ya kukidhi vigezo vya Bodi ya Mfuko wa Mikopo ya Nyumba za Watumishi wa Serikali.
Kauli hiyo imetolewa leo mjini Dodoma na Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi Mhe. William Lukuwi wakati akiwasilisha bungeni hotuba ya makadirio ya mapato na matumizi kwa mwaka ujao wa fedha.
Alisema kuwa Serikli imekamilisha uhakiki wa maombi mapya 191  ya watumishi wa umma waliomba mkopo wa nyumba katika maeneo mbali.
Mhe. Lukuwi aliongeza kuwa kati ya maombi hayo watumishi 181 yamekidhi vigezo vya mfuko huo na yanatarajiwa kuidhimishwa mwishoni mwa mwezi huu.
Aidha , alisema kuwa Serikali kupitia Watumishi Housing Company (WHC) imeanza kujenga nyumba za kuuza kwa watumishi wa umma katika mikoa ya  Morogoro, Dar es salaam, Pwani, Tanga  na Mwanza
Mhe. Lukuwi alisema kuwa watumishi wa umma wanaotaka kununua nyumba hizo wanawaweza kupata mikopo yenye mashrti nafuu kupitia Benki za Azania , CRDB, NMB, BoA na Exim zilizoingia makubaliano na Watumishi Housing Company wanaojenga nyumba kwa ajili ya kuwauzia watumishi wa umma katika maeneo mbalimbali nchini.

No comments:

WIZARA YA ARDHI YAPONGEZWA KUTENGA FEDHA KUKAMILISHA MRADI WA MAKTABA

Kamati ya Bunge ya Ardhi, Maliasili na Utalii imeipongeza Wizara ya Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi kwa kutenga fedha kiasi cha Shiling...