CHAMA cha Mapinduzi (CCM) kimewataka Wajumbe wa Baraza la Wawakilishi Zanzibar kuendelea kushirikiana ili kuunda nguvu ya pamoja itakayosaidia kuharakisha maendeleo ya nchi kwa ufanisi zaidi.
Kimesema utendaji mzuri wa viongozi hao ndani ya Baraza hilo ndiyo utakaoweza kukirahisishia kazi Chama cha Mapinduzi katika uchaguzi mkuu wa 2020, hali itakayojenga imani kwa wananchi kuirejesha tena CCM madarakati kutokana na utendaji mzuri wa viongozi hao.
Akizungumza Naibu Katibu Mkuu wa CCM Zanzibar, Nd. Vuai Ali Vuai wakati akibadilishana mawazo na Katibu Mpya wa Kamati ya Wawakilishi wa Chama cha Mapinduzi ndani ya Baraza la Wawakilishi Zanzibar (Mnadhimu) huko Afisi Kuu ya CCM Kisiwandui Mjini hapa.
Nd. Vuai alimpongeza kiongozi huyo kwa kuaminiwa na Wajumbe wa Baraza hilo na kumchagua kuwa Mnadhimu wa Wawakilishi wote wa CCM ndani ya Chombo hicho cha kutunga sheria za nchi.
Alisema kuchaguliwa kwa Mnadhimu huyo pamoja na msadizi wake kutasaidia kuongeza ufanisi wa kusimamia vyema shughuli za baraza la wawakilishi ili ziende sambamba na mahitaji ya wananchi majimboni.
Alieleza kwamba mbali na viongozi hao kuwa na jukumu la kuandaa miswaada, kutunga sheria na kupitisha Bajeti za nchi bado wana wajibu wa kusimamia kwa vitendo ilani ya Uchaguzi ya CCM ya 2015/2020 pamoja na kulinda maslahi ya Chama hicho.
No comments:
Post a Comment