Sunday, May 22, 2016

NAPE ATOA WITO WA WA ELIMU YA UOKOAJI IFUNDISHWE MASHULENI


 Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Mhe. Nape Nnauye akizungumza wakati wa kuangalia mazoezi ya uokoaji majini yaliyofanywa na vijana 50 waliohitimu mafunzo ya uokoaji yaliyodhaminiwa na Flaviana Matata Foundation pamoja na UTT wakati wa maadhimisho ya kumbukumbu ya miaka 20 tangia kuzama kwa meli ya MV. Bukoba yaliyofanyika mjini Mwanza ambapo mamia ya watu walifariki akiwemo mama mzazi na binamu wa Flaviana Matata.
 Sehemu ya waliofuzu mafunzo ya uokoaji wakionyesha namna ya kuokoa watu majini wakishuhudiwa na Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Mhe. Nape Nnauye, Mhe. January Makamba Mbunge wa Jimbo la Nyamagana Mhe. Stanslaus Mabula na Flaviana Matata
 Sehemu ya makaburi ya pamoja ya waliofariki kwenye ajali ya MV. Bukoba mwaka 1996 ambapo leo imetimia miaka 20 tangia ajali hiyo imetokea.
 Viongozi wa Dini walioshiriki kwenye kutoa ibada maalum ya kumbukumbu ya miaka 20 tangia kutokea kwa ajali ya MV. Bukoba.
 Sheikh Hassan Kabeke akiongoza dua wakati wa maadhimisho ya kumbukumbu ya miaka 20 ya ajali ya MV. Bukoba ambapo mamia ya watanzania walifariki dunia.
 Flaviana Matata (kushoto) akiwa amejiinamia kwa huzuni wa kumbukumbu ya ajali ya MV.Bukoba ambapo alipoteza Mama Mzazi pamoja na Binamu, katikati ni Kaimu Meneja Mkuu wa Kampuni ya Huduma za Meli Kepteni Winton Mwasa na kulia ni Waziri wa Habari, Utamaduni Sanaa na Michezo Mhe. Nape Nnauye.
 Mchungaji Obadi Ruralila wa KKT akiongoza ibada ya kuwaombea marehemu kwenye kumbukumbu ya miaka 20 tangia kuzama kwa meli ya MV. Bukoba ambapo mamia ya wakazi wa jiji la Mwanza wakiongozwa na Flaviana Matata walijitokeza kwenye makaburi ya pamoja ya Igoma mjini Mwanza.
 Shemasi John Kasembo wa Parokia ya Ilemelea akitoa neno la mungu wakati wa kilele cha kumbukumbu ya miaka 20 tangia kuzama kwa meli ya MV. Bukoba.
 Kaimu Meneja Mkuu wa Kampuni ya Huduma za Meli Kepteni Winton Mwasa akizungumza machache juu ya uboreshaji wa elimu ya uokoaji waliyoitoa kwa kushirikiana na Flaviana Matata Foundation pamoja na UTT ambapo watu 50 walihitimu mafunzo ya kuokoa majini.
 Flaviana Matata akizungumza wakati wa kumbukumbu ya miaka 20 ya ajali ya kuzama kwa Meli ya MV Bukoba ambapo alipoteza Mama Mzazi pamoja na Binamu yake.
 Mbunge wa Jimbo la Ilemela akizungumza kwenye maadhimisho ya miaka 20 ya jali ya kuzama kwa meli ya MV. Bukoba.
 Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Mhe. Nape Nnauyeakizungimza wakati wa maadhimisho yamiaka 20 ya kumbukumbu ya ajali ya MV. Bukoba ambapo alisema imefika wakati elimu  uokoaji itolewe kwa vijana wadogo ili wawe na uelewa mkubwa wa kukabiliana na matatizo yanapotokea.
 Sehemu ya wakazi wa jiji la Mwanza ambao walipoteza ndugu , jamaa na marafiki wa
 Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Mhe. Nape Nnauye(kushoto), Flaviana Matata na Waziri wa Nchi, Ofisi ya Makamu wa Rais, Mazingira na Muungano January Makamba wakiweka shada la maua kwenye kaburi la pamoja ikiwa sehemu ya maadhimisho ya miaka 20 ya kumbukumbu ya kuzama kwa meli ya MV. Bukoba.
 Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo  Mhe. Nape Nnauye pamoaja na Waziri wa Nchi, Ofisi ya Makamu wa Rais, Mazingira na Muungano January Makamba wakijiandaa kuwasha mishumaa.
 Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Mhe. Nape Nnauye(kushoto) akiweka mshumaa kwenye kaburi pamoja na Flaviana Matata kwenye maadhimisho ya miaka 20 ya kuzama kwa MV. Bukoba ambapo mamia ya watu walipoteza maisha.
 Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Mhe. Nape Nnauye(kulia) akimsikiliza  Flaviana Matata muda mfupi kabla ya kupiga picha ya pamoja za kumbukumbu ya maadhimisho ya miaka 20 ya kuzama kwa meli ya MV. Bukoba.
Picha ya Pamoja.

No comments:

WIZARA YA ARDHI YAPONGEZWA KUTENGA FEDHA KUKAMILISHA MRADI WA MAKTABA

Kamati ya Bunge ya Ardhi, Maliasili na Utalii imeipongeza Wizara ya Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi kwa kutenga fedha kiasi cha Shiling...