Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Bandari Tanzania (TPA) Injinia Alois Matei akiwaeleza waandishi habari kuhusu mradi wa maboresho ya Bandari ya Dar es Salaam utakaogharimu kiasi cha Dola za Marekani milioni 690 ambapo mradi huo unafadhiliwa na Serikali, Benki ya Dunia,Trade Mark East Afrika na DFID, kulia ni Afisa Mawasiliano Mwandamizi wa Mamlaka hiyo Bw. Focus Mauki na mwisho Kapteni Abdullah Mwingamno wa TPA Bandari ya Dar es Salaam.
Mhandisi Mkuu wa TPA Bi Mary Mhayaya akitoa ufafanuzi kuhusu mradi wa Flow meter mpya ya Kigamboni ambao umeshakamilika na hivyo kuwezesha mafuta yote yanayoingia nchini kupitia Bandari ya Dar es Salaam kupimwa na kujulikana kiasi halisi kilichoingizwa hapa nchini ili kuiwezesha Serikali kupata mapato stahiki ikiwemo kodi .
Baadhi ya waandishi wa habari wakifuatilia taarifa ya Mamlaka ya Bandari TPA iliyokuwa ikitolewa na Kaimu Mkurugenzi wa Mamlaka hiyo Injinia Alois Matei kwenye ukumbi wa Idara ya Habari Maelezi leo.
No comments:
Post a Comment