Thursday, May 26, 2016

MATUNDA YA MSAADA WA NHC WA MASHINE ZA TOFALI KWA VIJANA YAJIONYESHA


Jengo la ofisi ya kikundi BYDEMCOS  lipo ndani ya kata ya Bulyanhulu  Kakola kwenye ukaguzi uliofanywa na NHC Shinyanga wa maendeleo ya vikundi vya vijana vilivyopewa msaada na Shirika la Nyumba la Taifa mkoa wa Shinyanga. Ukaguzi umefanyika wa vikundi vyote ambavyo vilikabidhiwa mashine hizo na kutembelea shughuli wanazozifanya.  Kila Halmashauri ilipewa msaada wa mashine nne (4) ambazo, kila mashine ina uwezo wa kuhudumia vijana wapatao kumi (10) na kila Wilaya ina kundi la vijana arobaini (40). Kwa maana hiyo, Shirika limesaidia ajira za moja kwa moja kwa vijana wapatao 6,720 katika Halmashauri hizo 168 kwa kutoa mashine 672 za kufyatulia tofali ambao nao wataweza kuzalisha ajira zipatazo 200,000 kutokana na kazi za ujenzi zitakazofanyika kwa kutumia matofali wanayotengeneza.


Meneja wa Shirika la Nyumba Mkoa wa Shinyanga, Ramadhani Macha akiwa na wanakikundi wa Iboja Ufundi Group katika Halmashauri ya Ushetu.
Jengo la ofsi ya kata  ya Nyamilangano  kama linavyoonekana ndilo litakalotumika  kwa kuanzia ofisi ya Mkurugenzi wa Halmashauri ya Wilaya Ushetu.
Kikundi cha Iboja ufundi Group kikifyatua tofali 27,000 kwa ajili ya ujenzi wa Ofisi ya Kata ya Nyamilangano, ambayo itaanza kutumika kama ofisi ya Mkurugenzi wa Halimashauri ifikapo Julai 2016  
Nyumba ya kawaida na inajengwa na kikundi cha vijana  kiitwacho vijana tujenge pamoja, kazi zote vijana hawa wanafanya kuanzia kufyatua tofali mpaka kujenga.
Jengo hili ni la  Kanisa Katoliki, lipo eneo  la  majengo Kahama  tofali zilizotumika kujengea  jengo hili zimefyatuliwa na kikundi cha UWAJUKA na tujiajiri  na mkandarasi yeye akafanya kazi ya ujenzi  na  Kanisa hili limetumia tofali elfu kumi na saba.

Moja ya kazi ambayo imefanywa na kikundi cha hapa kazi tu  kuanzia tofali mpaka na kujenga jengo la fremu za maduka, jengo hili lipo nyuma ya Chuo cha Veta mkoani Shinyanga.
Wa pili kutoka kushoto ni Afisa Maendeleo ya Jamii  Manispaa ya Shinyanga aliye vaa blue na anayefata wa kike ndie mmiliki wa nyumba hiyo.




Moja ya nyumba iliyojengwa na kubuniwa kwa ushirikiano wa vikundi vyote vilivyoko ndani ya halmashauri ya Manispaa ya Shinyanga, nyumba hii ina vyumba vitatu na  sebule na mpaka hapo ilipofikia imegharimu kiasi cha Sh 12,000,000 ikiwa  imepigwa plasta ndani hivyo mafundi hawa wanasema nyumba hii itagharimu 20 milioni itakapokuwa imekamilika kila kitu.

No comments:

WIZARA YA ARDHI YAPONGEZWA KUTENGA FEDHA KUKAMILISHA MRADI WA MAKTABA

Kamati ya Bunge ya Ardhi, Maliasili na Utalii imeipongeza Wizara ya Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi kwa kutenga fedha kiasi cha Shiling...