Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Nyumba NHC
Bw. Nehemia Mchechu Kyando akizungumza na wageni waalikwa wakati wa hafla ya
uzinduzi wa uuzaji wa nyumba za mradi wa 711 uliopo Kawe jijini Dar es Salaam,
Nyumba hizi ziko kwenye majengo 8 yenye ghorofa 18 kila moja ambayo
yanatarajiwa kuchukua watu 1000 kwa na huu ni utangulizi wa ujenzi
wa mji mpya wa kisasa unaotarajiwa kujengwa eneo la Tanganyika Packers Kawe
jijini Dar es salaam ambao ukikamilika utaweza kuchukua watu 15,000.
Watu wanaohitaji kununua nyumba hizo
wanatakiwa kufika ofisi za NHC Kinondoni au Makao Makuu ya Shirika la Nyumba
NHC Upanga au wanaweza kutembelea kwenye mtandao wa shirika hilo kwa maelezo
zaidi ili kununua nyumba hizo hafla ya uzinduzi wa nyumba hizo ilifanyika
mwishoni mwa wiki katika makao makuu ya shirika hilo Upanga.
Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Nyumba NHC
Bw. Nehemia Mchechu Kyando akizungumza na wageni waalikwa wakati wa hafla ya
uzinduzi wa uuzaji wa nyumba za mradi wa 711 uliopo Kawe jijini Dar es Salaam.
Meneja wa Mauzo wa NHC, Tuntufye
Mwambusi akizungumza na Monica Joseph Mkurugenzi wa Kampuni ya Monifinace
Investment Group Limited wakati wa uzinduzi huo.
Meneja wa Mauzo wa NHC,
Tuntufye Mwambusi akimsikiliza Bw. David Shambwe Mkurugenzi wa Hazina na Maendeleo
ya Biashara NHC katika uzinduzi huo kulia ni Mwita Makenge Mkurugenzi wa
Kampuni ya Wegmar Limited na kushoto ni William Genya Meneja Maendeleo ya
Biashara NHC .
Mkurugenzi wa Shirika la Nyumba la Taifa
NHC Bw. Nehemia Mchechu katikati na Felix Maagi, Mkurugenzi wa Fedha wa
NHC wakimsikiliza Linley Kapya kutoa Benki ya NBC wakati alipokuza akizungumza
jambo katika uzinduzi huo.
Meneja wa Mauzo wa NHC, Tuntufye
Mwambusi akizungumza na kuelezea jinsi mradi huo utakavyokuwa na mambo muhimu
yaliyopo katika mradi huo huku akiwa na baadhi ya wafanyakazi wa shirika hilo.
Baadhi ya wafanyakazi wakipozi kwa picha
wakati wa hafla hiyo
Meneja wa Mauzo wa NHC,
Tuntufye Mwambusi akifafanua jambo mbele ya waalikwa wakati
alipokuwa akiuelezea mradi huo.
Baadhi ya wageni walikwa wakifuatilia
maelezo mbalimbali kuhusu mradi wa 711 wa Kawe jijini Dar es Salaam.
Meneja Masoko wa Shirika la Nyumba la
Taifa NHC Bw. Arden Kitomari akifafanua mambo mbalimbali wakati akiuelezea mradi
wa 711 uliopo Kawe jijini Dar es Salaam.
Wageni waalikwa wakifuatilia maelezo
yaliyokuwa yakitolewa na maofisa mbalimbali wa Shirika la Nyumba NHC
Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Nyumba NHC
Bw. Nehemia Mchechu pamoja na wafanyakazi wa shirika hilo wakifuatilia video
zilizokuwa zikionyesha jinsi mradi huo utakavyokuwa wakati wa uzinduzi
uliofanyika Makao Mkuu wa shirika hilo Upanga.
Baadhi ya wageni waalikwa kutoa taasisi
mbalimbali wakifuatilia uzinduzi huo.
Kutoka kulia ni Meneja wa Mauzo wa
NHC, Tuntufye Mwambusi na Meneja Masoko wa NHC Bw. Aden Kitomari wakimsikiliza
Taji Liundi aliyekuwa MC wa uzinduzi huo.
Wageni mbalimbali walihudhuraia uzinduzi
huo.
No comments:
Post a Comment